Katika kunogesha na kuleta msisimko katika tamasha lake la kutimiza miaka 13 ya muziki wake na uzinduzi wa albamu yake ya sita tangu kuanza muziki, mwanamuziki Judith Wambura au Lady Jaydee ametangaza rasmi kwamba kila atakayehudhuria onyesho lake na kulipa kiingilio, atatoka na nakala ya albam yake hiyo albamu ya bure.
Jaydee kwa kushirikiana na wanamuzki wenzake Joh Makini, Grace Matata, Profesa jay, Hamza Kalala na bendi yake ya Machozi Band, wanatarajia kufanya onyesho kubwa katika maegesho ya mgahawa wake uitwao Nyumbani Lounge usiku wa tarehe 31 May, ameiambia mwananchi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika.
Akiiongelea albamu yake hiyo aliyoipa jina la Nothing But The Truth, amesema si albam ambayo kijana aliye katika harakati anapaswa kuikosa, maana humo ndani ameelezea kwa kiasi kikubwa changamoto za kimaisha na jinsi ya kukabiliana nazo kama kijana.
Nyimbo ambazo zilishatangulia kwenye albamu hiyo ni pamoja na Yeye, Joto Hasira ambao amemshirikisha Profesa Jay na Yahaya ambao atautoa siku moja baada ya uzinduzi wa albamu hiyo.
Naye Meneja wa mwanamuziki huyo, ambaye pia ni mumewe, Gadner G Habash amewahakikishia wapenzi wa muziki wa LadyJaydee kwamba siku hiyo kutakuwa na mjumuisho wa burudani za tangu mwanamuziki huyo anayeongoza kwa kuwa na tuzo nyingi kwa upande wa wanamuziki wa kike anaanza muziki.
CHANZO: Mwananchi
No comments:
Post a Comment