Friday, 24 May 2013

Mtanzania atwaa medali dhahabu Romania


Mary Naali

Na Imani Makongoro, Mwananchi

 Mwanariadha wa Tanzania, Mary Naali ametwaa medali ya dhahabu mbio za nusu marathon (km 21) ‘Bucharest International Half Marathon’ zilizofanyika nchini Romania.
Naali anayetokea klabu ya African Ambassadors Athletics (AAAC) ya Arusha alitumia saa 1:16:32 kumaliza mbio hizo zilizokuwa na ushindani mkubwa.
Mkimbiaji wa Ethiopia, Salome Albere alikamata nafasi ya pili akitumia saa 1:18:20, wakati Nicoleta Petrescu wa Romania akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 1:20:24 kumaliza mbio hizo.
Mkenya Kirui Nicholas aliibuka kinara upande wa wanaume kwenye mbio hizo akitumia saa 1:04:07 na Andrew Lesuuda aliyetumia saa 1:04:53 na Japhet Kanda aliyetumia saa 1:07:12 wote kutoka Kenya wakihitimisha tatu bora.
“Medali hii ni zawadi kwa taifa langu, nimepambana hadi mwisho kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri japo ushindani ulikuwa mkali,” alisema Naali.
Naali anashikilia rekodi ya kutwaa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika New Delhi, India mwaka 2010.  

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...