Saturday, 18 May 2013

LISTENING PARTY YA ALBUM "NOTHING BUT THE TRUTH"



Mara nyingi wasanii wengi wakishamaliza kurekodi Albums
Kabla hazijafikia hatua ya kwenda sokoni.
Hufanya party inayojumuisha wadau na marafiki mbali mbali
Kupata nafasi ya kuzisikiliza nyimbo zote kabla hazijaanza kuuzwa.

Kwa maana hiyo basi
Jumamosi hii ya tarehe 18 MAY 2013
Patakuwa na Party maalum ya kusikiliza nyimbo zote zitakazopatikana kwenye album ya sita ya Lady JayDEE "Nothing But The Truth"

Hafla hiyo itafanyika NYUMBANI LOUNGE jijini Dar es salaam
Na kutakuwa na kadi za mialiko maalum 200
Ila wengine wote wanaopenda kujumuika mnakaribishwa kwa kiingilio cha sh. 5,000/= mlangoni

DJ Kim atakuwepo kukurusha Oldies kwenye Saturday Boogie Down
Kuanzia saa 3:00 usiku yaani 9:00pm mpaka watu wakitosheka

Karibuni sana mpate nafasi ya kipekee ya kusikiliza nyimbo za JayDee kwanza, kabla hazijatoka.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...