Uongozi wa Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) leo umemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji wao
mpya, Mama Mizinga Melu. Mama Melu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Standard Chartered Zambia, ambapo aliongoza benki hiyo kwa Miaka 6 kabla
kuhamia NBC.
Mizinga si mgeni
kwenye sekta ya kibenki, kwani keshashika nafasi kubwa mbali mbali akiwa na Benki ya Standard
Chartered. Nafasi hizi ni kama vile Mkuu wa Kimataifa wa Mashirika ya
Maendeleo, Uingereza ambapo alikuwa anasimamia maendeleo ya mikakati na
utekelezaji, pamoja na kuwa Mkuu wa Taasisi za Fedha nchini Kenya na Afrika
Kusini, Kanda ya Afrika.
Mama Melu si
mgeni kwa Tanzania, kwani alishawahi kuwa Mkuu wa Hazina katika Benki ya
Standard Chartered Tanzania kati ya mwaka 2000 na 2003. Kabla ya kushika nafasi
hiyo alifanya kazi kama kaimu Mkuu wa Hazina Benki ya Standard Chartered Uganda
mwaka 1998 na Zambia mwaka 1999.
Mizinga ana
Shahada ya Pili (Masters) ya usimamizi wa Biashara (MBA) kutoka Chuo chaHenley
Management College (Uingereza) na ni mwanachama wa Taasisi ya wafanyakazi wa
mabenki(ACIB), pamoja na sifa nyengine mbali mbali.
No comments:
Post a Comment