Thursday, 23 May 2013

MTWARA LEO



Barabara ikiwa imefungwa




Baadhi ya nyumba zikiwa zimechomwa moto

Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
-Barabara zimewekwa vizuizi, magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita. 
-Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
- Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao.  Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
-Mahakama ya mwanzo ya Mitengo nayo imechomwa moto.
-Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali  Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
-Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari Magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
-Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigwi mfululizo.
-Mabasi matano ya Champion yaliyobeba wanajeshi yako njiani yanaelekea Mtwara.
-Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
-Bunge laahirishwa tena kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
-RPC aongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende kazini. Lakini kiuhalisia hali bado sio shwari.

CHANZO: Mtwara kumekucha blog

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...