Tuesday, 28 May 2013

UNALIFAHAMU KABILA LA WAHIMBA KUTOKA NAMIBIA?


Leo tuangalie kabila la Wahimba kutoka Namibia.Kabila hili linaishi kaskazini mwa Namibia.Wahimba ni wafugaji.


Wanawake ndiyo wafanyakazi wakubwa katika jamii kama kubeba maji na kujenga nyumba. Wanaume hujishughulisha na maswala ya siasa na sheria.Wahimba hujifunga kitambaa kidogo.Wanawake hujipaka mchanganyiko wa majivu,siagi na udongo (ochre) kwaajili ya kujikinga na hali ya hewa ya jangwa.
Mitindo ya nywele huonyesha madaraja yaani kama ni watoto,wanaume walioa au wanawake walioolewa n.k.Wahimba ni watu wanaomwabudu Mungu mmoja -Mukuru pamoja na mababu wa ukoo.Mukuru anabariki tu, wakati mababu wanaweza kubariki na kulaani.
Wahimba ni kabila linalofuata mila kama wamasai.






No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...