Tuesday, 28 May 2013

NDOA ZA UTOTONI,SHERIA INASEMAJE?




Je,nini kinasababisha ndoa za utotoni?Sheria ya ndoa ya mwaka 71 imepitwa na wakati na ni wakati mwafaka sheria hiyo ibadilishwe kwani kwa mtazamo wangu nadhani ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo ya kuwa na ndoa hizi za utotoni.Sheria hii ina ruhusu binti wa miaka 15 kuolewa na mvulana wa miaka 18 kuoa.Je,kwanini msichana nae asiolewe akiwa na miaka 18?Binti wa miaka 15 ni mtoto kabisa huyu.Kwa kweli sheria hii ni kandamizi na haifai katika ulimwengu huu wa sasa.Wale wanao husika na ubadilishwaji wa sheria imefika wakati wa kufanyia kazi sheria hii ili kukomesha unyanyasaji huu kwani wasichana wengi wamenyimwa haki zao kama watoto!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...