STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
Irene Uwoya |
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata.
Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za kibongo ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharabia sifa.
CHANZO: Global Publishers
No comments:
Post a Comment