Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
“Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
Akizungumza na mwandishi wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana wakaamua kufanya maulidi tu.
No comments:
Post a Comment