Monday 24 June 2013

IKULU YA MAREKANI YAWEKA NJE RATIBA YA OBAMA KUJA BONGO


Rais Barrack Obama
IKULU ya Marekani na Idara ya Habari (Maelezo), wametangaza ratiba ya Rais Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha kuwa atakaa siku mbili tu, kuanzia Julai Mosi na kuondoka kesho yake.
Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal na Afrika Kusini. Mara atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika upande wa Mashariki wa geti la kuingia Ikulu.
Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe Michelle pia siku hiyohiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na  wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika na Marekani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam. “Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,” ilisema taarifa ya Maelezo.

Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa atakayoandaliwa Ikulu na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete. Siku itakayofuata ataweka shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulizi la bomu mwaka 1998. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion na atatoa hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia Bara la Afrika kuzalisha nishati ya umeme.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...