Monday 24 June 2013

NMB YAFADHILI UMITASHUMTA MANISPAA YA SUMBAWANGA

1 (2)
Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku akimkabidhi  Afisa Elimu, Modesta Zambi sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye UMITASHUMTA  manispaa ya Sumbawanga.Makabidhiano haya yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.Benki ya NMB imefadhili UMITASHUMTA kwenye manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni tisa. Lengo kuu la ufadhili huu ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza  vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
DSC09476Sehemu ya mipira iliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili  ya UMITASHUMTA.Picture 008
Maofisa wa Benki  ya NMB  na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia)  mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...