Wednesday 26 June 2013

JE,NI JUKUMU LA NANI KUWASAIDIA VIJANA KUACHANA NA MADAWA YA KULEVYA?



Masikini kijana huyu akijidunga
Kwasasa vijana wengi wameathirika na madawa ya kulevya.Tumeshuhudia jinsi familia zilivyopoteza vijana wao kutokana na tatizo hili.
Je,nini ni sababu za kuongezeka kwa utumiaji wa madawa ya kulevya?

  • Vijana wengi hujiingiza katika tatizo hili kutokana na shinikizo kutoka kwa marafiki, yaani walianza kutumia madawa kwakuwa wengi wa marafiki wao walikuwa wakitumia.
  • Ukosefu wa ajira hupelekea wengi kujiingiza katika tatizo hili kwani kwa kutokuwa na chochote cha kujishughulisha hupelekea vijana kugeukia madawa ya kulevya.


Utumiaji wa madawa ya kulevya usiodhibitwa, huleta athari  kwa mtumiaji.Athari hizo ni:
  • MaradhiHii ni athari kubwa ya madawa ya kulevya. Kuna maradhi mengi ambayo vijana hawa wanapata kutokana na madawa haya. Baadhi yao wamepata matatizo ya akili. Maradhi haya yanawapata vijana hawa kwa kasi mno kwa sababu ya kutokula vyema.Pia wanaambukizana maradhi kwa kubadilishana sindano. Hii imesababisha kusambaa kwa UKIMWI.
  • Uhalifu: Vijana wengi wanaotumia madawa ya kulevya hawana ajira,na madawa haya huuzwa hivyo ili wapate pesa za kununulia ni lazima wawaibie wananchi wengine.
  • Kifo: Mwisho wa watumiaji wengi wa madawa ya kulevya ni kifo.Hii hutokana na athari wanazozipata kutokana na kutumia madawa haya.
NINI KIFANYIKE?
Jukumu la kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya ni letu sote.Madawa haya ni biashara inayofanywa na watu.Bunge litunge sheria kali kuhusu madawa ya kulevya na kuhakikisha wanaokamatwa na kuthibitika sheria inachukua mkondo wake.Serikali izipe ushirikiano taasisi zisizo za kiserikali zinazohusika na kusaidia vijana walioathirika na madawa ya kulevya kwani zinafanya kazi iliyotukuka ila kasi bado ni ndogo sana.
Vijana wanaotibiwa na kuachana na madawa wasaidiwe katika kuanzisha shughuli za kijasiriamali ili waweze kurudi katika maisha ya kawaida.Wanaweza kupatiwa elimu ya ujasiriamali,hapa serikali ibuni mkakati.

KWA HAKIKA TUKIPAMBANA TUTAWEZA!

Anna Nindi


No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...