Wednesday 26 June 2013

SEHEMU YA 1: RISITI NI HALALI KWA MNUNUZI AU NI MATWAKWA YA MUUZAJI?

Je,wananchi tunaelewa umuhimu wa risiti tunaponunua bidhaa?Hivi,muuzaji anapoacha kukupa risiti na wewe ukaondoka kwa amani kabisa unajua nini madhara yake?
Nimeamua kuandika kuhusu hii mada kutokana na uzoefu wangu mwenyewe.
Mwaka jana mwezi wa novemba nilinunua vifaa vya ujenzi katika duka moja(jina kapuni) mjini Tanga.
Tulikwenda dukani na kaka yangu.Kwa kuwa orodha ilikuwa ndefu na vitu vyao waliviweka hapa na pale,tuliwaachia wenye duka orodha yetu ili watoe vitu vyote na tungevipitia baadae.Tuliwauliza itawachukua muda gani kutoa vitu vyote,na walitupa muda wao na sisi tukawaambia kuwa tutarejea saa ngapi.
Kutokana na kuwa na shughuli nyingi baadae mimi sikurudi tena dukani bali kaka yangu alikwenda mwenyewe.Alikuta wametoa vitu vyote,vingine wameweka wanavyotaka wao ambavyo sisi hatukuchagua ila hili si la maana.Kaka yangu aliwauliza risiti ipo wapi wakamjibu tumempa dereva.Kaka yangu akidhani risiti kapewa dereva akatoka na kuingia ndani ya gari na kuondoka.Alipofika nyumbani nikamuuliza risiti ipo wapi?Akanijibu anayo dereva.Nikamwambia amwambie anipe.Alipomuuliza dereva kuhusu risiti akasema yeye hajapewa.
Itaendelea kesho.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...