Thursday, 6 June 2013

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KITUO CHA KUREKEBISHA TABIA KWA WANAWAKE NA WASICHANA WATUKUTU CHA PERTAPIS HUKO SINGAPORE.

IMG_5786
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo cha watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati alipokitembelea kituo hicho tarehe 6.6.2013. Mama Salma yupo nchini Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi. IMG_5796
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na uongozi wa kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu cha Pertapis kilichoko nchini SingaporeIMG_5840Mwenyekiti  wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.














No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...