Thursday, 6 June 2013

UKUMBI WA STEREO KINONDONI WATEKETEA KWA MOTO MCHANA WA LEO

 Gari la zimamoto likiwa eneo la tukio likizima moto ulioteketeza Ukumbi wa Stereo leo mchana. Mashuhuda wa liokuwepo eneo hilo walisema kuwa moto huo ulioanza majira ya saa nane mchana umeelezwa kuwa umetokana na hitilafu ya umeme iliyoanza baada ya kutokea cheche za moto wakati mmoja wa wapambaji alipokuwa akiendelea na kazi ya kupamba ukumbi huo kwa ajili ya sherehe iliyokuwa ifanyike ukumbini hapo leo jioni. 

Mashuhuda wengine walitonya kuwa baada ya moto huo Mtungi wa gesi uliokuwa jikoni pia ulilipuka na kuongeza kasi ya moto huo. Aidha imeelezwa kuwa baada ya moto huo, gari la zimamoto liliwasili eneo la tukio baada ya dakika 20 ulipotokea moto huo lakini, liliondoka bila kufanya kazi hiyo ya kuzima moto baada ya kufika eneo hilo na kujikuta halina maji na hivyo likaondoka kwenda kujaza maji na kurejea tena.
 Hapa ni kwenye kona ya ukumbi huo kama inavyoonekana.
 Mamia ya wananchi wakishuhudia moto huo ukiteketeza ukumbi huo.
 Mmoja kati ya waliojitokeza kusaidia kuzima moto akimwaga maji ndani ya ukumbi huo kumalizia kuzima moto.



 Akizima moto wa mwisho mwisho

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...