Mwanajeshi wa Marekani anayetuhumiwa kutoa zaidi ya nyaraka 700,000 za siri kwa tovuti ya Wikileaks anafikishwa mahakamani leo (jana) mjini Maryland akishtakiwa kwa kuvujisha taarifa hizo za siri.
Kuruta wa ngazi ya kwanza Bradley Manning (pichani) mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na uwezekano wa kifungo cha maisha bila msamaha iwapo atapatikana na hatia kwa kuvujisha nyaraka hizo mwaka 2010, hali ambayo iliikasirisha serikali ya Marekani.
Manning anakabiliwa na mashataka 21, ikiwa ni pamoja na shitaka baya zaidi la kusaidia adui, pamoja na kukabiliwa na hukumu chini ya kifungu cha kupambana na ujasusi cha mwaka 1917.
Mahakama ya kijeshi ya Fort Meade, Maryland , kiasi ya kilometa 50 kaskazini mashariki ya mji wa Washington, inatarajiwa kuendesha kesi hiyo hadi karibu mwishoni mwa mwezi August.
No comments:
Post a Comment