Singapore imesema itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kuinua elimu na kuongeza ujuzi kwa watanzania zaidi kupitia mpango wake wa kutoa fursa za mafunzo kwa nchi zinazoendelea.
Rais wa Singapore Dkt. Tony Tan Keng Yam amesema hayo wakati alipozungumza na rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete katika ikulu ya Singapore.
Rais huyo wa Singapore amesema nchi yake haina rasilimali, hivyo imewekeza zaidi katika elimu na mafunzo ya kuanzia shuleni, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu na kuwa iko tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja hiyo.
Rais Kikwete alifanya ziara ya siku tatu nchini Singapore akitokea Japan ambako alihudhuria mkutano wa Tokyo unaozungumzia maendeleo ya Afrika.
Akiwa nchini Singapore rais Kikwete alikutana na kuzungumza na wafanyabiashara na kuwakaribisha kuwekeza nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment