Thursday, 6 June 2013

UINGEREZA KUWAOMBA RADHI NA KUWAFIDIA WALIOTESWA WAKATI WA HARAKATI ZA MAUMAU NCHINI KENYA

MAU MAu
Serikali ya Uingereza huenda ikaomba msamaha na kuandaa fidia kwa waliokuwa wanachama wa harakati za ukombozi wa Kenya Mau Mau.
Waliokuwa wanachama wa kundi hilo waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma waliodai kutendewa na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.

Mwezi Oktoba mwaka 1952 ukoloni wa Uingereza nchini Kenya ulitangaza hali ya hatari na kuanzisha harakati za kijeshi zilizolenga vuguvugu la Mau Mau.
Kundi hilo lilikabiliana vikali na majeshi ya Uingereza likipinga kunyang’anywa ardhi na kutaka uhuru wa kujitawala.
Miongo kadhaa baadae wanachama wa kundi hilo walionusurika wamekuwa na vita vingine ambapo walifika katika mahakama ya London na kuwasilisha madai wakitaka Uingereza iwaombe radhi na kuwafidia kwa dhuluma walizotendewa.
Wakati huo huo leo jijini Nairobi nchini Kenya linafanyika kongamano la kitaifa linalohusu jinsi ya kuhamasisha jamii umiliki na matumizi ya ardhi.
Kongamano hilo linaongozwa na muungano wa kutetea masuala ya umiliki wa ardhi nchini humo National Lands Alliance.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...