Thursday, 6 June 2013

HALI ILIVYOKUWA BAADA YA KHADIJA KOPA KUPEWA TAARIFA YA KUFIWA NA MUMEWE

Mkuu wa mkoa wa Rukwa  Eng.Stella Manyanya (kushoto) akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho, Khadija Kopa alipokuwa kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki dunia leo alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere mkoani Rukwa jana.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda 


No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...