Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Jackson Midala na Afisa Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde wakionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mita mpya za malipo ya maji kadri unavyotumia (LUKU) ambazo wateja wa shirika hilo watafungiwa. Mita hizo zimezinduliwa jana Jijini Dar es Salaam ambapo wateja wa Dawasco pia wanaweza kulipia kupitia AirtelMoney.
Wawakilishi wa mabenki katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam.
Wawakilishi wa mitandao ya mawasiliano katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam.
Shirika La Maji Safi Na Maji Taka Dar Es Salaam (Dawasco) ndio lenye jukumu la kutoa huduma ya Majisafi na uondoshaji wa Majitaka katika Jiji la Dar Es Salaam na miji iliyoko Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Dawasco imejipanga kumfikishia mteja huduma za malipo kwa technolojia ya kisasa popote alipo ndani na Nje ya Tanzania kupitia huduma za Kibenki na Simu ya Kiganjani.
Hivyo basi Dawasco inazindua rasmi Mfumo wa Malipo ya ankara za Maji ulioanza rasmi kutumika Tarehe 01.07.2013 Katika vituo vyake vyote 13. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha huduma kwa Mteja. Pia mfumo utasaidia kupunguza msongamano wa muda mrefu uliokuwepo wa kulipia Madirishani na utampa mteja njia mbalimbali za kulipia Bili yake na kwa wakati wowote.
Mfumo huu pia utamsaidia Mteja kufanya malipo sehemu yoyote nje ya Jiji la Dar es salaam na hata nje ya Nchi
Malipo kwa njia ya Benki yatafanyika kwenye tawi lolote katika Benki zifuatazo: CRDB – A/C No. 01J1021921900, BARCLAYS- A/C No. 0014003711, BANK OF ( BOA) –A/C No. 02022460009 na NMB No. 20103300047
Mteja atakwenda Benki anayotaka kufanya Malipo na kujaza Fomu ya fedha (deposit Slip). Mteja ahakikishe ameandika namba ya account ya Dawasco kwa usahihi ikifuatiwa na kiasi cha fedha anacholipia, kisha kurudisha fomu kwa karani wa Benki kwa Malipo.
Huduma za kibenki kwa kutumia simu za kiganjani ni kwa Wateja Wenye Akaunti Katika Benki za; CRDB, NMB, BENKIYA POSTA, AKIBA COMMERCIAL BANK (ACB) Na EXIM BANK.
Malipo kwa kutumia Simu ya kiganjani yatafanyika Kupitia M-PESA, AIRTEL MONEY, TIGO PESA, Na ZANTEL EZY PESA.
Pia malipo kwa ankara za Maji zinafanyika kupitia ATM ZAUMOJA SWITCH, huduma ya SELCOM na MAXMALIPOinayopatikana kwa Mawakala waliopo kila kona ya Jiji La Dar Es Salaam.
Aidha kuna matawi ya Benki yako karibu na vituo vya Dawasco hivyo wateja wa maeneo husika watapata urahisi wa kufanya Malipo yao ya kila mwezi na kuondoa usumbufu wa kwenda mbali zaidi. Matawi hayo ya Benki yaliyo karibu na Vituo vya Dawasco ni haya yafuatayo:
Kituo cha Dawasco Temeke kilichopo Temeke Usalama kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Temeke Hospital, CRDB– Quality Centre
Kituo cha Dawasco Kawe kilichopo njia panda ya Kawe kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB yaliyopo MbeziBeach, Kijitonyama, Mikocheni na MlimaniCity na matawi ya NMB yaliyopo MlimaniCity, MbeziBeach na Mwenge na Tawi la BOA Bank iliyopo Sinza
Kituo cha Dawasco Tabata kilichopo Dar West kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB Tabata Magengeni.
Kituo cha Dawasco Kimara kilichopo kimara mwisho (Matankini) kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Ubungo Mwisho, CRDB-Mbezi Stand Mpya, CRDB-Mlimani City, NMB, BANK OF AFRICA (BOA) zilizoko Ubungo Plaza, CRDB Ubungo Stand, ATM ZA UMOJA SWITCH-zilizopo Mbezi Suka
Kituo cha Dawasco Kinondoni kilichopo nyuma ya jengo la Airtel kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Namanga/Msasani, ATM ZA UMOJA SWITCH- Mwanamboka,AKIBA COMMERCIAL na CRDB zilizopo Millenium Tower Makumbusho
Kituo cha Dawasco Magomeni kilichopo Magomeni Mapipa kipo karibu na Matawi ya Benki ya BARCLAYS- Magomeni Mapipa na NMB-Magomeni Mikumi.
CHANZO: Mo blog
No comments:
Post a Comment