Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye, akisakata rhumba katika ‘Send Off’ ya Natasha.
Imelda Mtema na Hamida Hassan
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye, mwishoni wa wiki iliyopita aliinogesha sherehe ya kuagwa ‘Send Off’ ya mwigizaji wa kitambo na Mtangazaji wa Radio Times, Suzan Lewis ‘Natasha’.

Waziri mkuu huyo aliambatana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Hemed Kipozi, katika Uwanja wa Mnazi Mmoja ilipofanyika sherehe hiyo iliyopewa jina la ‘Natasha Night’.
Sumaye pamoja na viongozi wengine hawakuwa nyuma katika kulisakata rhumba pale zilipopigwa nyimbo za zamani ‘zilipendwa’. ‘MC’ aliwataka wageni waalikwa kujumuika pamoja na kupanda jukwaani kwa ajili ya kuserebuka, nao hawakujivunga.
Mbali na Sumaye na Kipozi, mastaa mbalimbali wa filamu wa hapa nchini walijitokeza kumpa kampani mwenzao.
Katika sherehe hiyo iliyokuwa na shamrashamra na vitu vingi vya kuvutia kila wakati wageni waalikwa walionekana kujawa na nyuso za bashasha.
Katika sherehe hiyo iliyokuwa na shamrashamra na vitu vingi vya kuvutia kila wakati wageni waalikwa walionekana kujawa na nyuso za bashasha.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment