Ubuyu.
Na Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kutangaza kwamba mafuta ya ubuyu hayafai kwa matumizi ya binaadamu, taarifa hiyo imewafanya watu wengi kukumbwa na hofu ya vifo vya ghafla.

Mafuta ya ubuyu.
Hofu hiyo inatokana na kuamini kwa muda mrefu kwamba mafuta hayo yamekuwa ni tiba asilia na salama kwa magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana mahospitalini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya 37 jijini Dar Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza alisema mafuta hayo yana tindikali ya mafuta hivyo hayafai kutumiwa kama chakula na binaadamu.

Simwanza alioongeza kwamba binaadamu anayetumia mafuta hayo kama dawa yuko hatarini kupatwa na kansa za aina tofautitofauti.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baadhi ya wakazi wa mjini hapa wamesema kama hivyo ndivyo, basi vigogo wengi watakuwa matumbo joto kuanzia sasa.
“Kweli waheshimiwa wengi ndiyo watakaoumia kwa kuwa ndiyo wananunuzi wakubwa wa mafuta hayo,” alisema mkazi wa Majengo, Rashid Mussa.
Naye Albert Martin alishangazwa kupigwa marufuku kwa mafuta hayo sasa.
“Siku zote hao TFDA walikuwa wapi, mafuta ya ubuyu yametangazwa sana na yameuzwa kwa uwazi iweje leo yapigwe mafuruku?” alihoji.
Awali ilidaiwa kuwa mafuta ya ubuyu yanatibu saratani za aina zote, yanatibu ugonjwa wa kisukari, yanatoa sumu mwilini, yanapunguza kitambi na yanakinga mwili kwa kuongeza CD-4 na magonjwa mengine.
Afisa Mwelezaji Biashara wa Sido mkoani hapa, Batuza Moshi alisema kwamba taarifa za TFDA zichukulie kama ndiyo sahihi kwa sasa.
“Nilikuwa nalifuatilia suala hilo ni kweli katika mafuta ya ubuyu kuna kemiko ambazo siyo nzuri, hivyo lazima tujiulize zinatoka wapi?”
Hata hivyo, Batuza alisema kwamba lazima kuna sehemu inakosewa kwani hata Afrika Kusini wanazalisha bidhaa hiyo.
“Isingekuwa rahisi kwa Afrika Kusini kutengeneza mafuta hayo kama yana madhara,” alisema Batuza.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment