MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Swahiliwood Wema Abraham Sepetu ndiye msanii anayelipwa fedha nyingi kuliko msanii yoyote wa filamu katika kushiriki katika filamu kutoka kwa watayarishaji wengine ili uweze kumshirikisha Wema Sepetu katika filamu yako kama mwigizaji bila kujali anacheza scene ngapi gharama yake ni milioni kumi.
Wema ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake ya utengenezaji wa filamu Swahiliwood inayojuklikana kwa jina la Endless Fame Film anasema kuwa moja ya sababu inayomfanya aweze kuchaji gharama hiyo inajumuisha na kutumia kampuni yake pamoja yeye mwenyewe kuigiza katika filamu hiyo, kwa hiyo ni wajibu wa mhusika kumudu gharama hizo.
.
”Yah, kama mtayarishaji ananihitaji kushiriki katika filamu yake atatakiwa kunilipa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa kushiriki katika filamu yake, lakini pia kuzingatia ratiba ya utendaji usiingiliane na kazi zangu nyingine,”anasema nyota Wema.
Inasemekana kuwa Wema ndio msanii wa kike anayeuza filamu kuliko mwigizaji wa filamu wa kike, pengine ndio sababu ya kuweza kutoza gharama kubwa katika kushiriki filamu nje ya kampuni yake unapomuhitaji Wema kwa ajili ya mapatano unaongea na mtendaji wake wa karibu Chiddy Classic.
Gharama hizo ndio kubwa kwani hadi sasa msanii ambaye amelipwa kwa kiwango cha juu ilikuwa ni milioni tano ikiwa kama ndio kikomo cha malipo kwa wasanii wenye majina na wamiliki wa makapuni yao, msanii kama Ray the Greatest hanunuliki kwani si rahisi kushiriki nje ya kampuni yake ya RJ Company.
No comments:
Post a Comment