Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-SACCOS, Naibu Kamishna wa Polisi, Thobias Andengenye. Ngao hiyo alikabidhiwa jana kama ishara ya IGP kuwa balozi wa saccos hiyo katika viwanja vya kilwa road wakati wa uzinduzi wa Tawi la URA-SACCOS la Kilwa Road.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini , IGP Saidi Mwema akipasha na maofisa, wakaguzi na askari wa Jeshi la Polisi, wakati wa uzinduzi wa Tawi la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi Kilwa Road, Ura-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Kilwa Road la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bahati nasibu ya kushindania pikipiki na cherehani itakayochezeshwa na Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, Ura Saccos tawi la kilwa road. Tawi hilo lilizinduliwa na IGP.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi, Advera Senso akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOSS. Ngao hiyo ni ishara ya kuwa balozi wa SACCOS hiyo ambayo tawi lake la Kilwa Road lilizinduliwa jana na IGP.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Jeshi la Polisi wakionyesha mahadhi ya makhirikhiri jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tawi la Kilwa Road la Chama cha kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOS.Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi
---
Na Alex Mpeka, Jeshi la Polisi.
Askari wametakiwa kutumia huduma zinazotolewa na Chama cha ushirika cha akiba cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (Ura- Saccos) ili kujijiendeleza katika ujasiliamali pamoja na kuboresha maisha yao.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema jana wakati wa mahadhimisho ya miaka saba (7) ya Ushirika huo, yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Kurasini barabara ya Kilwa, jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa askari wanapopata mikopo katika ushirika huo wanakuwa hawana wasiwasi wa kutozwa riba kubwa kwa kuwa ushirika huo lengo lake ni kuinua ustawi wa askari na familia zao.
IGP Mwema, alisema kuwa, Jeshi la Polisi hivi sasa linaendelea kutekeleza program ya Maboresho, ambapo kupitia ushirika huo na kuweza kutoa jumla ya shilingi billioni arobaini na mbili (42), ambazo zimetumika kwa ajili ya kuboresha maisha ya askari na familia zao kwa lengo la kujiendeleza kielimu, ujenzi wa nyumba ununuzi wa viwanja, kujikimu pamoja na ujasiliamali.
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Thobias Andengenye, alisema kuwa, miongoni mwa mafanikio yametokana na ushirikiano mzuri wa Benki ya CRDB ambapo watendaji wa URA SACCOS wameweza kuendesha mafunzo na kuandaa semina mbalimbali za kuwajengea uwezo na kufuata misingi ya sheria na taratibu za sera ya vyama vya ushirika.
Aidha katika maadhimisho hayo, IGP Mwema alizindua bahati nasibu ya weka akiba na ushinde ambapo kupitia bahati nasibu hiyo wanachama wake watapata fursa ya kushidania vyerehani kumi, pikipiki tano aina ya boxer ambapo mshiriki atatakiwa kuwa na akiba ya isiyopungua laki tano katika akaunti yake.
Pamoja na mambo mengine IGP Mwema aliwakabidhi ngao mabalozi sita kutumia nafasi walizo nazo kunadi URA SACCOS ambao ni Kamishina wa Polisi Zanzibar (CP) Mussa Alli Mussa, Mkuu wa chuo cha Polisi moshi (MPA) Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Matanga Mbushi, Mkuu wa chuo cha polisi dar es salaam, Ally Lugendo, Mkurugenzi wa Muziki wa Jeshi la Polisi, Kamishina msaidizi (ACP) Haule, pamoja na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso
Chama cha Ushirika cha kukopa cha Jeshi la Polisi (URA- SACCOS) Kilianza mwaka 2006 na mpaka hivi sasa kimetimiza miaka saba ambapo kimeweza kuboresha maisha ya askari na watumishi raia wanaofanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ukilinganisha na benki zingine za kibiashara.
No comments:
Post a Comment