Usafiri wa pikipiki maarufu kama ``boda boda`` hutumika na wengi katika sehemu mbalimbali barani Afrika.Ni usafiri mzuri kama usalama ukizingatiwa. Tatizo tulionalo ni kuwa usafiri wa boda boda hauzingatii kabisa usalama wa abiria na dereva bila kusahau sheria za barabarani(sina uhakika maana wakipakiza mshikaki sijui kama wanakamatwa au la).Boda boda nyingi zimekuwa zikipakiza abiria zaidi ya mmoja,maarufu kama ``mshikaki`` bila kujali usalama wa waliopanda pikipiki hiyo.Unakuta boda boda imepakia watu watano na hakuna aliyevaa kofia ya kujilinda na ajali,au unakuta ni dereva tu ndiye amevaa kofia ya kujilinda na ajali.Hivi wadau, bodaboda ina uwezo wa kubeba watu wangapi?Je,boda boda ina uwezo wa kubeba watu zaidi ya bajaji?Mimi hapa sielewe na ndiyo maana kwangu naona boda boda ni JANGA kama hazitatumika kwa kuzingatia vigezo vya usalama barabarani.
Hebu angalia aina za mishikaki katika picha hapa chini.Kuna mshikaki wa watu watatu, wanne,watano n.k
Boda boda in Kenya
Boda boda in Kampala
Boda boda Kampala
Boda boda, Sudan
Familia katika boda boda ,Uganda!
No comments:
Post a Comment