Saturday, 7 September 2013

DK. MENGI: VIJANA WENGI WANAWEZA KUWA MATAJIRI


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ambaye ni muasisi wa shindano la kutuma ujumbe kwa njia ya ku-tweet kwenye akaunti yake ya tweeter @regmengi, kuhusu namna mbalimbali za kuondoa 

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema Tanzania  inaweza kuinuka kiuchumi na kuwa na vijana wengi matajiri, endapo kundi hilo litakuwa na uwezo wa kuibua mawazo bora ya kibiashara.

Dk. Mengi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwazawadia washindi watatu wa shindano lake la Tweet na Mengi, lenye lengo la kuibua mawazo mapya ya kibiashara kwa vijana wajasiriamali.

Washindi wa shindano hilo kwa mwezi uliopita ni Lilian Wilson mshindi wa kwanza, Suzan Senga wa pili na Ombeni Kaaya aliyeshika nafasi ya tatu.

Alisema Tanzania ina tatizo la vijana wasio na mbinu za kuibua mawazo bora kutokana na kukosa chombo cha kuwasaidia kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika na Ulaya.

Alitaka kuwepo na jitihada maalumu za kuwasaidia kwa ajili ya kuondoa umasikini uliopo miongoni mwa wananchi, ambao hawakustahili kuwa na hali hiyo duni kutokana na nchi kuwa na raslimali nyingi na za kutosha.

"Naamini kwa miaka michache inayokuja kama vijana watakuwa na tabia ya kuanzisha mawazo na kuomba uwekezaji, tutazalisha vijana matajiri 100 kila mwaka," alisema Dk. Mengi.

Alisistiza kwamba mtu anaweza kupata mafanikio baada ya kutelekeleza ndoto yake kubwa kwa kutumia mtaji mdogo na sio vinginevyo.

"Wengi hawaoni fursa na kutojiamini kwa kile wanachotaka kukifanya, badala yake wanakimbilia kuomba mitaji na kuishia kupata hasara," aliongeza kusema.

Kwa upande mwingine aliomba serikali na viongozi mbalimbali kufungua milango kwa kuhakikisha vijana wengi wanafanikiwa katika uwekezaji mdogo wa kibiashara kwenye mawazo yao.

Ushindi wa vijana hao watatu  ulitokana na kujibu swali la Dk. Mengi, linalouliza njia gani ifanyike kuzalisha ajira nyingi kwa ajili ya vijana hapa Tanzania?

Mshindi wa kwanza alijinyakulia Sh. 1,000,000, wa pili alipata Sh. 500,000 na watatu aliondoka na kitita cha  Sh.300,000.

Aidha, swali la mwezi huu linauliza "raslimali za nchi hii zinawezaje kutumika kuongeza ajira kwa vijana?"
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...