Monday 7 October 2013

KUTANA NA MWANAHARAKATI WA KUGOMBEA HAKI ZA MTOTO WA KIKE KUTOKA MAREKANI ALIYETUA DAR




Anaitwa Zuriel Oduwole, msichana mdogo wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, yupo jijini Dar es salaam  akiwa na wazazi wake na wadogo zake watatu, katika harakati zake za kupigia chapuo umuhimu wa kumuendeleza mtoto wa kike katika Afrika. 
Tayari Zuriel ameshafanya mahojiano na Marais wanane (akiwemo Rais Kikwete) pamoja na Waziri Mkuu wanne wa Afrika, pamoja na mfanyabiashara tajiri kuliko wote Afrika Bw. Dangote, hali kadhalika nyota wa tennis duniani toka Marekani, Venus na Serena Williams.
Zuriel, ambaye ni mtengeneza filamu, mwanahabari na mwanaharakati wa maslahi ya wasichana wadogo,  yuko nchini akitokea Malawi ambako kama ilivyokuwa huko, hapa nchini, hususan jijini Dar es salaam, atafanya mihadhara katika shule kadhaa kuhamasisha wasichana wadogo wajiamini na kusaidia katika kuzungusha gurudumu la maendeleo huku wakipiga vita unyanyapaa dhidi yao. Mwezi Agosti mwaka huu Zureil aliweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote waliopata kuhojiwa na jarida maarufu la watu maarufu na matajiri duniani la Forbes. 
 Zureil akimhoji Rais wa Liberia Mhe Mama Ellen Johnson Sirleaf
 Zureil akimhoji Rais wa Nigerai Mhe Goodluck Jonathan


 Zureil akimhoji Mhe Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Zuriel akiongea na Rais Jakaya Kikwete
Zuriel akimhoji Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Salva Kiir Mayardit
CHANZO: Full shangwe

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...