Thursday, 10 October 2013

LINEX AMRUDISHA ADAM KAZINI



Katika wakati huu ambapo soko la video za muziki Tanzania limeingia ushindani mkubwa, Kila msanii akiwa anataka kufanya hatua ya ziada ili kuifanya video yake iwe ya kipekee zaidi, Msanii Linex Sunday Mjeda kwa upande wake amefanikiwa kumtafuta Dir Adam Juma na kufanya naye kazi ambaye kwa mujibu wake, ni ya gharama ama bajeti kubwa kuliko zile ambazo ziliwahi kutokea.

Linex amesema kuwa, video hii ni ya ngoma yake ya Kimugina na ameamua kufungia macho gharama zake ili kuifikisha katika ngazi za kimataifa, na mpaka sasa kazi imeshakamilika na ambapo amesema kuwa Adam amekubali kufanya naye kazi kwasababu ni moja kati ya wasanii ambao anawakubali uwezo wao na pia kazi hii imekuwa na bajeti ya kipekee ya ya kujitoa sana ili kupata kitu bora.

Baada ya kumbana saaaana, Line amesema pia kuwa, katika video hii ameamua kufunga macho na kumlipa model Jackie Cliff shilingi milioni 2 taslim ili kufanya naye kazi, Na Directoa Adam Juma akichukua kitita mara mbili zaidi ya gharama yake ya kawaida ambayo amekuwa akiwatoza wasanii kwa video, na hii inakuja sambamba na location ya aina yake.



 
CHANZO: EATV

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...