Saturday, 14 December 2013

Kijiji cha Qunu champokea Mandela

Jeneza la Mandela

Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.

Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa mda.
Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili.

Kijiji cha Qunu

Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...