Saturday 14 December 2013

MWANAMUZIKI MAARUFU HAPA NCHINI ''LADY JAYDEE'' AUGUA GHAFLA....ALAZWA HOSPITALI YA PRIMIER



Mwanamuziki mwenye jina kubwa katika Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ hivi karibuni aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake Kimara-Temboni, Dar na kukimbizwa katika Hospitali ya Primier Care iliyopo karibu na nyumbani kwake.
Akizungumza na paparazi wetu, ‘hazibandi’ wa staa huyo ambaye pia ni meneja wake, Gadna Habash ‘Kapteini’ alisema kuwa ‘waifu’ wake huyo
alipata maambukizi katika koo lake hivyo akatumia dawa ambazo hazikustahili.
Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ akichezea simuHospitali ya Primier Care.
Gadna alifunguka kuwa baada ya kutumia dawa hizo zilimletea homa kali ndipo walipomkimbiza katika hospitali hiyo na kugundua kuwa alitumia dawa ambazo hazikustahili kwa tiba ya koo hivyo walimlaza na kumuanzishia dozi nyingine.

“Mwanzo hata sisi tuliogopa sana kwa sababu alikuwa na homa kali lakini tulipomfikisha hospitalini waligundua kuwa alitumia dawa ambazo siyo tiba ya tatizo lake ambazo ndizo zilimdhuru, lakini hivi sasa yuko sawa na anaendelea na shughuli zake,” alisema Kapteini ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha Radio Times FM.
CHANZO: Kapingaz

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...