Monday 16 December 2013

MUME AKUSUDIA KUMTOA MKEWE ROHO HUKO MBEZI BEACH DAR

Bwana mmoja huko mbezi beach amemrudisha mkewe nyumbani ajiwa mahututi badala ya kumpeleka hospital kubwa ya Mwananyamala kama rufaa ilivyoandikwa na madaktari wa Masana Hospital iliyoko Mbezi jijini Dar (Afande Jaina Msangi, kushoto, dada wa mgonjwa Ramla kulia kwa mgonjwa, mimi mbele ya mgonjwa wakati tukimbeba kwa ajili ya kumpeleka Mwananyamala. Kushoto kabisa ni mume wa mgonjwa akiwa pembeni kabisa
Ni ngonjwa aliyezidiwa sana, hapo tumemshika alishwe chakula...kabla ya kumpeleka Mwananyamala Hospital.
Huyo ndo Mume wa mama Linda Mgonjwa, hapo akituambia hataki presha kama tunataka kumpeleka hospital tumchukue....baada ya vuta nikuvute ya kumtoa mgonjwa nyumbani apelekwe mwananyamala hatimae tulifanikiwa, na huyu mzee hajaenda kumuona tangu ampeleke.

Wakati tunahangaika kumbeba mke wake tumweke kwenye gari, yeye hatoi kabisa ushirikiano ndo kwanza yupo buze na mambo yake.
Tukamkomalia ndo akasaidia.!!!
Nikamuulia NIA yake ya kumrudisha Mgonjwa asiyejitambua tena ni Mke wake, alikuwa na Lengo gani?
Hapa ndo nyumbani kwa huyu mzee na mke we Linda Msoka. Huyu mama mpaka sasa ni mfanyakazi wa Hazina. Huyo gumegume alikuwa anafanyakazi Kiwanda sijui gani inavyoonekana mama ndo yuko vizuri kiuchumi, na mpaka sasa ni mfanyakazi wa Hazina lakini analala njaa yeye na huyu binti anaemsaidia Haya majumba mazuri jamani yana tabu? Heri sie tunakaa tandale kwa Amani
Linda Amekaa Mwananyamala siku sita leo siku ya saba tumemwamishia Muhimbili. Huyu mzee mume wake kaja siku mbili tu kati ya hizo siku sita, jana tulimwambia kwamba mgonjwa atahamishiwa Muhimbili akasema hataki usumbufu kama anahamishiwa huko yeye haimuhusu.... HIVI HUYU MZEE ANA AKILI SAWASAWA KWELI?
CHANZO: Wanawake live

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...