“Hali ya mitikisiko tena mikubwa mikubwa ambayo husababisha
maumivu mwilini, inaweza kuwa chanzo cha watalii kukoma kutembelea
hifadhi, hivyo mtainyima Serikali pato,” alisema Koroso.
PICHA|MAKTABA
Musoma. Watalii wanaotembelea Hifadhi ya Serengeti wanaweza kupungua kutokana na miundombinu ya barabara za hifadhi hiyo kuwa mbovu, imeelezwa.
Akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara juzi, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Mara, EmmanuelKoroso alisema mwenye jukumu la kuzitengeneza na kuzikarabati barabara hizo ni Hifadhi ya Serengeti.
Korosso alisema barabara hizo zinaweza kuwa chanzo kikuu cha watalii kukataa kutembelea hifadhi hiyo, kwa sababu hakuna sehemu ambayo mtalii anaweza kukaa kwa utulivu.
Alisema hivi sasa barabara hizo zitikisa wasafiri tangu mwanzo hadi mwisho.
“Hali ya mitikisiko tena mikubwa mikubwa ambayo husababisha maumivu mwilini, inaweza kuwa chanzo cha watalii kukoma kutembelea hifadhi, hivyo mtainyima Serikali pato,” alisema Koroso.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, John Ng’oina alisema barabara hizo wamekuwa wakizikarabati kwa gharama kubwa, lakini zimeendelea kuharibika, hivyo alishauri wahusika kunusuru mapato ya Serikali.
Ng’oina alisema kinachotakiwa ni kuweka barabara za lami, au mawe kama hifadhi zingine ambazo zina ardhi isiyofaa kukarabati kwa changarawe.
“Udongo wa hifadhi mlisema haufai kukarabati, sasa sioni sababu ya kuendelea kukarabati kwa udongo bali tafuteni njia mbadala ya ujenzi wa barabara hizo ikiwa ni njia ya kuendelea kuwavutia watalii,” alisema Ng’oina.
Naye Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa aliwataka wahifadhi hao kuangalia njia mbadala baada ya kufanya utafiti njia itakayotumika kuboresha barabara hizo.
“Badala ya kuendelea kuharibu fedha nyingi kukarabati barabara huku watalii wakiendelea kulalamikia barabara, sasa tafuta njia mbadala ambazo zitasaidia kuondoa kero hii,” alisema Tupa.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment