Wednesday 1 January 2014

BREAKING NEWS: WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA AFARIKI

Waziri wa Fedha William Mgimwa enzi za uhai wake.

Waziri wa Fedha, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa, William Mgimwa amefariki dunia leo akiwa hospitali ya Mediclinic Kloff, Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa!
Marehemu Mgimwa alizaliwa Januari 20, 1950 na amefariki akiwa na umri wa miaka 63.
Alipata Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Alisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Fedha (MBA) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...