Sunday 5 January 2014

Rapper EVE kufunga ndoa na mbunifu wa mitindo wa Uingereza, avishwa pete ya uchumba

Rapper mkongwe wa kike kutoka Marekani Eve Jihan Jeffers ‘EVE’ amethibitisha kuwa amechumbiwa rasmi, na hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni mbunifu wa mitindo wa Uingereza Maximillion Cooper.
Cooper n Eve
Eve na Cooper wamekuwa wapenzi kwa takribani miaka mitatu sasa.
Cooper alimwomba uchumba EVE mwenye miaka 35 siku ya Christmas ya mwaka jana 2013 huko Edinburgh, Scotland walipoenda kusheherekea sikukuu.



EVE na Cooper
Kama wafanyavyo wasichana wengine wanapoingia katika status ya ‘uchumba’, EVE aliionesha pete yake ya uchumba ya almasi kupitia Instagram na kuandika,
“Asante kwa kila mmoja kwa pongezi zenu za engagement! Tulitaka kusheherekea na familia yetu na marafiki kwanza kabla ya kutangaza”.
Eve na familia
Eve akiwa na mama yake na kaka yake, tayari pete ya uchumba ikiwa kidoleni

Baadaye mchumba wake naye aliandika kupitia ukurasa wake “Yes it’s official…I asked the question…and she said YES! WAHOOO! we’re getting married!”.
Hii itakuwa ni ndoa ya kwanza kwa Eve, wakati mume wake mtarajiwa tayari ana watoto wanne waliopatikana katika ndoa zake zilizopita
CHANZO: BONGO5

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...