Kundi maarufu la muziki wa Kwaito la nchini Afrika kusini, Mafikizolo linatarajia kuwasili leo jijini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya onesho moja tu linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Jumamosi ya April 5.
Mafikizolo imekuwa na rekodi nzuri ya kushinda kwenye tuzo mbalimbali za muziki, kutokana na kupiga muziki na kucheza kwa umahiri, hasa mtindo wao maarufu wa Kwaito. Kundi hilo linaloundwa na wasanii wawili, Nhlanhla Nciza na Tebogo Madingoane na kwa sasa linaendelea kutamba na vibao kama “Khona” na “Happiness”.
CHANZO: Bongo5
No comments:
Post a Comment