Huwezi kujua ukali wa mamba kama hujavuka mto. Jijini Dar nilitumia usafiri wa aina zote isipokuwa bodaboda tu.Hii ni nzuri ili kujua wananchi walio wengi wanaishi vipi. Ilikuwa ni uzoefu mzuri kwani nilijifunza na kuona mengi yanayojiri katika barabara zetu na katika vyombo vyetu vya usafiri wa jumuiya.
Kwa kweli usafiri ni changamoto kubwa katika jiji la Dar.Hali hii inachangiwa na barabara nyingi kuwa katika matengenezo ya maandalizi ya njia za mabasi yaendayo kasi. Foleni zimeshamiri karibia kila kona ya jiji. Ni kitu cha kawaida kughairi safari kabla ya kufika kwani uhakika wa kufika na kurudi mapema huwa haupo.Hii ndiyo hali ya usafiri katika jiji la Dar kwasasa.
Ndani ya UDA
Picha na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment