Tupo njiani tukielekea Wilaya ya
Pangani,mkoani Tanga. Baada ya kupita eneo la Duga, mbele kidogo, tunakuta
kundi kubwa la watu wakiwa wamekusanyika.
Palikuwa na zogo kubwa.Dereva tuliekuwa nae
alisimama na kuuliza nini kilikuwa kinaendelea. Mmoja ya watu aliyekuwepo
katika mkusanyiko ule akamjibu kuwa kuna wezi wa mbuzi wamekamatwa.
Tulipoangalia vizuri tukaona kuna watu wawili wamekalishwa chini huku wakiwa na
damu nyingi.
Inasemekana watuhumiwa hao walikutwa na ngozi
mbichi yenye rangi ya mbuzi aliyepotea hivyo kupelekea kushukiwa kuwa wao ndiyo
walikuwa wezi kwani ”anayekutwa na ngozi, ndiye aliyeiba mbuzi”!
KWELI TEMBEA UONE.
Mwandishi Anna Nindi
No comments:
Post a Comment