MAHITAJI
½ kjc giligilani nzima
½ kjc jeera(binzari nyembamba) nzima
1 kitunguu maji-kata vipande vidogovidogo
1kjc chumvi
½ kjc unga wa giligilani
½ kjc unga wa jeera
¼ kjc binzari
½ kjc pilipili ya unga/tandoori masala
¼ kjc unga wa cayenne
Vikombe 4-5 bamia iliyokatwa katika duara ndogo
4-5 Nyanya –kata vipande vidogovidogo
4 KJ mafuta ya mizeituni(olive oil) au mafuta
yeyote ya kupikia uyapendayo.
FANYA HIVI
Kaanga vitunguu na olive oil mpaka view rangi ya kahawia kwa
mbali. Moto
uwe wa mdogo wastani. Weka jeera na giligilani nzima na kanga kwa dakika 1. Weka bamia na changanya vizuri. Funika na acha kwa dakika 2.
Ongeza chumvi, pilipili ya unga/taandori masala, jeera ya unga, giligilani
ya unga, cayenne na binzari. Changanya vizuri na funika, acha iive kwa dakika
5-6 katika moto mdogo.
Mwisho,weka nyanya na pika kwa dakika 5. Bamia yako ni tayari.
Unaweza kula na wali, ugali n.k
MAANA YA VIPIMO VYANGU
kjc: Kijiko cha chai
KJ: Kijiko cha chakula
No comments:
Post a Comment