Hii ni moja kati ya juisi nizipendazo.Mabungo hulimwa Zanzibar ila
hupatikana Dar es salaam pia.
Tunda la bungo linavyoonekana. Hizi mbegu za ndani,
zikichanganywa
na maji,ndiyo hutengenezwa juisi.
MAHITAJI
Vipimo: Kupata takriban gilasi 6
3 Mabungo
6-7 glasi za maji
Sukari kiasi upendacho
*Chumvi kidogo sana (Chumvi hukata uchachu)
Juisi ya bungo
|
FANYA HIVI
1.
Kata mabungo na toa mbegu zake na weka katika mashine ya kusagia.
2. Weka
maji, sukari na chumvi usage kidogo tu.
3.
Chuja,mimina katika jagi weka katika friji.
4.
Mimina katika glasi na furahia juisi yako.
DOKEZO: Unaweza
kunywa juisi ya bungo kwa kitafunwa upendacho au na mlo upendao.Ni nzuri sana
ikinywewa ya baridi.
No comments:
Post a Comment