Ugemaji wa ulanzi
Ulanzi ni pombe ambayo hugemwa kwenye vitindi, au kwa jina lingine
kwenye mianzi midogo midogo ambayo haijakomaa, pindi tu inapochomoza kutoka
ardhini baada ya siku chache. Ulanzi unapogemwa kwa mara ya kwanza huwa mtamu
kama togwa
au juisi, lakini unapomaliza siku mbili, tatu au nne, huwa mkali. Ulanzi ni
pombe ya asili sana kwa wapangwa, maana ni jadi kwa wapangwa kunywa ulanzi.
Ulanzi unavyoonekana (picha na riziki yetu blog) |
Hata
watoto wadogo hupewa ulanzi kama juisi. Ulanzi kwa wapangwa, ni pombe ambayo inaheshimika
sana.
Wapangwa wanapokwenda shambani, huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka
Mfanyakazi shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya kazi, hadi apewe ulanzi.
Pia, hata katika harusi, sherehe za kimila kama vile kujengea
makaburi(MAHOKA), Mila za kumurudisha mjane nyumbani (NGOTORA), mila za kuabudu
miungu, n.k, Ulanzi ndio huwa unatumika hasahasa kuliko pombe nyingine.
Kwahiyo,Wapangwa wote kama vile KINA WILLAH, HAULE, MULIGO,
MTWEVE, NGAIRO, MWINUKA,n.k, ambao bado wanatii mila na desturi zao, Ulanzi
kwao ni jadi.
CHANZO: Wikipedia
No comments:
Post a Comment