PICHA: (Kwa hisani ya Tanzania today)
Wimbi la ajali limeendelea kuligubika taifa letu.Tumesikia na
kusoma ajali mbali na za kusikitisha zilizotokea hivi karibuni. Hii ni hali ya
kusikitisha sana kwani watu wasio na hatia wanapoteza maisha kutokana na uzembe
wa mtu mmoja tu,DEREVA!
Watoto wengi wanabaki yatima na kuongeza idadi ya watoto wa
mitaani, wanawake na wanaume wanabaki wajane, majeruhi wengi wanapata vilema
vya maisha kutokana na uzembe wa huyu DEREVA!
Hebu angalia picha hii mazingira ambayo dereva wa basi anataka kulipita lori!Sijui leseni wamepewa na nani hawa!PICHA: (Kwa hisani ya Full Shangwe)
Hivi huyu ni kweli DEREVA yupo juu ya sheria?
Hivi kweli hakuna kinachoweza kufanyika ili kupunguza kama si
kukomesha ajali hizi?Mimi binafsi nadhani kuna njia nyingi, zikiwemo za gharama
nafuu na za gharama kubwa.
Tukianza na njia za gharama kubwa ni kutengeneza barabara zetu
kuwa njia 2,yaani njia ya kwenda na njia ya kurudi. Hapa, hatutasikia tene
ajali za kugongana uso kwa uso.
Ni gharama kujenga barabara hizi lakini inawezekana maana kuna
pesa nyingi inatumika ndivyo sivyo na sina haja haja kuuelezea sana kuhusu hili
kwani natumaini kuwa kila mmoja wetu anajua.
Njia ya pili ambayo haina gharama kabisa ni kuwafungia/kunyang´anya
leseni madereva wote wanaosababisha ajali pamoja na kupewa adhabu ikiwemo za
kifungo na kulipa mali aliyoharibu.
PICHA: (Kwa hisani ya Habarika blog)
Dereva yeyote aliyefungiwa/kunyang´anywa
leseni asije kupewa leseni tena katika maisha yake. Adhabu hizi zote ziende
sambamba!
Hii itaweka heshima katika barabara zetu na kunusuru maisha ya
watu wasio na hatia.
Je mdau, wewe una mawazo gani? Tafadhali changia ili tuokoe
maisha ya watu wasio na hatia!
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment