Mito ya
kutupia katika makochi ni moja ya kirembesho katika sebule lako na hasa ikiwa
ipo katika rangi na mpangilio wa kibunifu. Mito hii ipo ya ukubwa na maumbo
tofauti kulingana na mahitaji ya mtumiaji. Muhimu ni kuangalia ukubwa wa
makochi yako ili ujue aina na ukubwa wa mito unayotaka.Rangi ya mito yako(katika
kuchanganyanmito) inaweza kuzingatia moja kati ya vitu hivi: rangi ya makochi
yako, rangi ya kuta za sebule lako, rangi ya mapazia yako au rangi ya zulia.
Mfano,kama
unaweka mito 3 katika kochi,unaweza mkto 1 kuwa na rangi ya mapazia, mto wa 2
rangi ya kochi na mto wa 3 rangi ya zulia. Hapa mdau ni swala la ubunifu tu!
Angalia
baadhi ya mito hapa kwa kupata uelewa zaidi.
No comments:
Post a Comment