Aliyewahi kuwa mmoja wa walimbwende nyota ambaye pia ni muigizaji, mwandishi wa vitabu na pia mtangazaji wa kipindi cha televisheni nchini Marekani, Trya Banks anatarajia kutua nchini Kenya wikend hii.
Ujio wa nyota huyo nchini Kenya ni muendelezo wa kutangaza kipindi chake kipya kinachohusiana na maswala ya kuwatafuta mamodo nyota barani Africa ambapo mpaka sasa majaji wa show hiyo wamekuwa wakifanya ziara mbalimbali barani humo kutafuta mamodo hao.
Hii itakuwa ni nafasi pekee ya mamodo nchini Kenya kuweza kuonyesha vipaji vyao ili kuweza kujitangaza kimataifa na kupata mikataba katika makampuni mbalimbali.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment