Saturday, 31 August 2013

AFRICAN PRINT WADAU

vlisco | two as one

Vlisco evening gowns made with fabrics from the ‘Delicate Shades’ collection

Vlisco -fashion that has a hot and mysterious strength in the designs. Read more http://africafashionguide.wordpress.com/2011/11/01/vlisco-delicate-shades-collection-illustrated/

TANZANIAN MUSIC - Q Chief feat. Barnaba & Linah - zamani ( Official Video)

20 kusomea gesi na mafuta China, Brazil


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kwenda nchini Brazil na China kusomea shahada ya uzamili fani ya mafuta na gesi. Picha na Fidelis Felix 

Dar es Salaam. Watanzania 20 wamepata ufadhili kwenda China na Brazil, kusoma shahada ya uzamili katika fani ya gesi na mafuta, huku Serikali ikieleza kuwa mpaka sasa kuna pengo la wataalamu zaidi ya 200 kwenye sekta hiyo.
Kuchaguliwa kwa Watanzania hao ni utekelezaji ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2013/14.

Hatma ya watuhumiwa wa dawa za kulevya JNIA Sept. 5


Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe
Hatma ya Maofisa wanne wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wanaodaiwa kuhusika kula njama kusafirishwa dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. bilioni 6.8 itajulikana Septemba 5, mwaka huu.

Maofisa wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo ni Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana. 


Mchungaji atoa siri alivyojihusisha na dawa za kulevya


Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kipentekoste la Kiinjili Tanzania, kwenye ofisi za gazeti hili wakati akitoa ushuhuda wa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya

Kinara wa kimataifa wa kuuza madawa ya kulevya aliyezunguka sehemu mbalimbali duniani kuuza mihadarati, ameacha biashara hiyo na sasa anahubiri Injili kupiga vita dawa hizo. Kigogo huyo Mtanzania na mzaliwa wa Mbeya, ambaye sasa anajiita kiumbe kipya katika Kristo, ni Mchungaji Macdonald Mwakisambwe wa Kanisa la Kipentekoste la Kiinjili jijini Dar es Salaam. 

ANGALIA JINSI JIDE ALIVYOTUNZWA NOTI BAADA YA KUIMBA WIMBO WAKE UNAOPENDWA KWASASA,``YAHAYA``


 Jide akikamua jukwaani.
Noti alizotunzwa Jide

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA UZINDUZI WA MOVIE YA LULU IITWAYO FOOLISH AGE

DSCN3364

Elizabeth Michael “Lulu” usiku wa 30/8 ameandika historia katika maisha yake ya movie kwa kuzindua movie yake mwenyewe kwa mara ya kwanza. Lulu amekuwa akifanya vizuri kwenye movie zinazoandaliwa na kampuni nyingine, lakini yeye binafsi hii ndiyo movie ya kwanza kuwekeza pesa zake. @hotlulumichael akiongea na waandishi wa habari alisema kwamba ameshiriki sana kwenye hii hasa kusaidia ku-direct na wazo zima la Foolish Age lilitoka kwa mtu wake wa karibu sana.
Uzinduzi ulifanyika kwenye hall la Mlimani City Conference center na kuhudhuriwa na wasanii kama Steve Nyerere,Joti,JB,Ray,Batuli,Monalisa na mama yake,JB,Wastara,Wema Sepetu,Jacklyne Wolper,Nisha na wengine wengi. Movie ilionyeshwa kwa dakika 20 na ikaanza kuuzwa palepale kwenye DVD moja yenye part 1 & 2
DSCN3334Hapa Lulu alijikuta mbele ya mic nyingi za waandishi wa habari
_MG_3451
DSCN3270Kemmy kutoka Kaole Sanaa Group, mmoja kati ya wasanii waliompokea Lulu wakati anaingia kwenye sanaa

SIKILIZA HEKAHEKA YA TAREHE 30 AUGUST 2013 KUTOKA CLOUDS FM NA GEA HABIBCHANZO: Millard Ayo

LULU AZINDUA FOOLISH AGE

Gari lililokuwa limembeba Lulu likiingia Ukumbini hapo.
Lulu akishuka ndani ya gari hilo tayari kwa kuzama ukumbini.Lulu akiingia ukumbini
Msanii wa Orijino Komedi Lucas Mhuvile 'Joti' (katikati), akishuhudia uzinduzi huo na marafiki zake.
Lulu akiongea jambo muda mfupi kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
Wema  na Kajala wakiselebuka moja ya ngoma za Lady Jaydee mala baada ya kuanza kutumbuiza.

KATUNI YA LEO

IGP aibiwa upanga wa dhahabu


Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema 
Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.

Friday, 30 August 2013

Michael Jackson - Rock With You

AIRTEL YATOSHA ; NYUMBA YA PILI ZIMEBAKI SIKU 5 TU!!!‏

Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha inayoshindaniwa.

Kikwete amlilia Askofu Kulola asema Tanzania imepoteza Mtumishi wa Mungu

Marehemu Dr. Moses KulolaTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Moses Kulola ambaye ameaga dunia , Alhamisi, Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 84.

Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulola. 

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.

“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”

Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zitatolewa siku ya Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa la EAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.   

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC,GOMA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                                             Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo  : DSM  22150463                                         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                                       DAR ES SALAAM,   29  Agosti, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                
--
1.       Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO

2.       Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. 

Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3.       MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.  
Dar es Salaam.

MSAKO MKALI

Chande Abdallah na Mayasa Mariwata
MSAKO mkali unaendelea kuvifumua vibanda vya video vinavyokiuka maadili kwa kuonesha mikanda ya ngono ‘X’ kwa watoto.
Baadhi ya DVD za ngono zilizonaswa.
Tukio la hivi karibuni limetokea Tandale Uzuri jijini Dar ambapo vijana wawili, Yasini Issa (25) na Kivuluga Abdi (27) wametiwa mbaroni kutokana na kudaiwa kuendesha biashara hiyo haramu.
Kabla ya tukio hilo, baadhi ya wazazi wanaoishi eneo hilo walipiga simu katika ofisi za gazeti hili wakilalamikia matukio hayo ya watoto kuoneshwa mikanda hiyo inayokiuka maadili ya Kitanzania.
Mmoja wa watuhumiwa akiondoa vifaa vyake kabla ya kuvipakia kwenye difenda.
Baada ya kupata ukweli wa tukio hilo, Jumatatu iliyopita waandishi wetu kwa kutumia kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), waliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Magomeni na kujipanga  kufanikisha zoezi la kuwatia mbaroni wahusika.
Upelelezi wa OFM uligundua kuwa kibanda hicho kilikuwa kikianza kuonesha mikanda hiyo michafu kuanzia saa mbili za usiku na kuendelea.  

NZOWA ATISHIWA KUUAWA!

Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
VITA kupinga madawa ya kulevya imeingia katika hatua nyingine, safari hii Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa amejikuta katika wakati wa hatari baada ya kutumiwa meseji za vitisho kwa maisha yake.

AFRICAN PRINT KWA SHUGHULI ZOTE HADI USHINDWE KUCHAGUA

photo miss16.jpg   Elegancy101 :: miss5.jpg picture by Nene_Aguzien - Photobucket

Vlisco evening gowns made with fabrics from the ‘Delicate Shades’ collection  Vlisco


WEMA: BILA KAJALA NAJIONA MTUPU

Na Imelda Mtema
KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.
Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”

PARADISE YA IRENE UWOYA

HIVI NDIVYO LAUNCHING VIDEO YA DIAMOND,MY NUMBER ONE ILIVYO HAPPEN NDANI YA SERENA HOTELWASAFI......WCB

Picha Picha tu zinahusika sehemu kama hizi.....Kumbukumbu tosha.


William Malecella or U can Call Him Lemutuz.....

DIAMOND AMFANYIA SUPRISE MZEE GURUMO KWENYE UZINDUZI WA VIDEO YAKE,AMPA GARI KAMA SHUKRANI YA MCHANGO WAKE KWENYE SANAA YA MUZIKI NCHINI TZ.
Nikizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa
nikiwa na Mzee Gurumo pembeni...

Mzee Gurumo akionesha Ufunguo juu baada ya kumkabidhi Gari kama
zawadi yangu kwake....

WALIOFUKUZWA TAZARA WAREJESHWAMkurugenzi Mkuu wa Tazara,Ronald Phiri

Mkutano wa bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) ,imetengua maamuzi ya kuwafukuza wafanyakazi 1,067 na kuagiza warudishwe kazini, agizo hilo linamtaka kila mfanyakazi kuendelea na kazi huku mishahara ikishughulikiwa.

MAJAMBAZI YAPORA SH 900 MILIONI BENKI ASUBUHI


Suleiman Kova 

Dar es Salaam. Watu wanane wanaodhaniwa kuwa majambazi, jana walipora zaidi ya Sh900 milioni katika Tawi la Benki ya Habib, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wizi huo ulitokea saa tatu asubuhi kwenye benki hiyo iliyoko makutano ya Mitaa ya Livingstone na Uhuru.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema fedha zilizoibwa ni Sh700 milioni na Dola za Marekani 181,885 (Sh285,444,000).
Kamanda Kova alisema wameanza kuwasaka majambazi hao waliohusika katika tukio hilo.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kova alisema majambazi hao walifika kwenye benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja na kujifanya ni wateja ambao walikuwa wamesindikizwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa sare za polisi.

SAA 4 ZAWATENGANISHA PACHA WALIOUNGANA


Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4. Picha na Michael Jamson 

Dar es Salaam. Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.
Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.

Thursday, 29 August 2013

PRESIDENT KIKWETE ARRIVES IN AUSTRIA,ATTENDS UN-EUROPEAN COMMISSION’S HIGH LEVEL RETREAT IN AUSTRIA

IMG_0041President Jakaya Mrisho Kikwete is welcomed by the Mayor of Salzburg, Mr Wilfred Haslauer at the Salsburg Airport in Austria on Thursday August 29, 2013 ahead of a High Level Retreat on “NEW IDEAS FOR A FAIR GLOBALISATION”. The retreat   is hosted and co-chaired by the President of the European Commission Mr Jose Manuel  Barroso and the UN Under-Secretary General for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator, Ms Valerie Amos. STATE HOUSE PHOTO
sa3The Tanzania flag flies alongside others of different countries at the Alpbach resort in Austria at the opening of the  High Level Retreat on “NEW IDEAS FOR A FAIR GLOBALISATION”. The retreat is hosted and co-chaired by the President of the European Commission Mr Jose Manuel  Barroso and the UN Under-Secretary General for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator, Ms Valerie Amos. STATE HOUSE PHOTO

START YOUR OWN ONLINE BUSINESS

 Many people are working online especially during this time of CoronaYou can do this also if you have a will.  Register for a Free Live Webi...