Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2013

JAMAA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR LEO NA KUGOMA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAISI KIKWETE

 Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela.
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo

STYLES: PANGILIA MAVAZI YAKO NA UTOKELEZEA NAMNA HII

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA NA NAIBU WAKE LEO IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.

HAPPY NEW YEAR WADAU WOTE WA RAINBOW-TZ BLOG!!!!!!!

Wafanyabiashara Mwanza wafunga maduka kupinga mashine za EFDs

Wafanyabiashara wa maduka Jijini Mwanza wakiingia mtaani wakipinga kupinga matumizi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs)

Wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja katikati ya Jiji la Mwanza, wamefanya mgomo wakipinga kupinga matumizi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs), ambazo hutolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Mgomo huo ambao ulianza saa 1:30 asubuhi, ulishika kasi katika barabara za Nyerere na Kenyatta kuelekea eneo la Makoroboi linalozunguka soko kuu, katikati ya jiji hilo, huku ukisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja , wananchi wa kawaida pamoja na uongozi wa serikali ya mkoa huo.

Kibamba: Hatutakubali Bunge la Katiba kutoonyeshwa live

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, ametahadharisha kuwa hawatakubaliana na mpango unaosukwa wa kutaka Bunge Maalum lisionyeshwe moja kwa moja.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa katika mkutano wa kuchagua wawakilishi wa Asasi zisizo za kiserikali ili majina yao yapelekwe kwa Rais kwa ajili ya kuyateua kushiriki kwenye Bunge Maalum la Katiba linalotarajia kufanyika Februari mwakani.

Jk: Bunge, wananchi wataamua Katiba

Rais Jakaya Kikwete amesema hatua inayofuata baada ya kukamilika kwa Rasimu ya Katiba ni maamuzi ya wananchi na Bunge la katiba ambayo yataifanya ipitishwe na kuwa Katiba kamili.
Kadhalika, Rais Kikwete alisema katika maamuzi hayo, viongozi wa kijamii na siasa wana nafasi kubwa ya kuhakikisha mchakato wa Katiba mpya unafanikiwa kwa kukwepa maslahi ya vyama vyao na makundi wanayotokea na kinyume chake Katiba ya sasa itaendele kutumika.

TOP 12 HOTTEST TANZANIAN ACTORS IN 2013

1. TINO
This year this vesertile actor performed well in movies like Mimi Na Mungu wangu and Kisate. Tino is one of great actors in our industry.


2. HASHIM KAMBI
Kambi appears mainly in supporting roles although sometimes he plays lead characters, and in those movies with strong supporting roles heroes and heroine get hard times from King Kambi in terms of performances. This year the actor crossed borders and starred in a Ghananian movie "Day After Death" with Van Vicker and John Dumelo. He will be seen again with Van Vicker in a Tanzanian movie in 2014. This year King Kambi looked fresh in movies like Fisadais, Foolish Age, Boss Tony. In short Kambi is one of Tanzanian actors who can essay Hollywood roles.

DUNIANI KUNA MAMBO: SHABIKI WA CHELSEA ALIYEISHI KWENYE HANDAKI MIAKA MINNE JIJINI DAR

Chacha Makenge akikaribisha wageni. Chacha akiongea na wageni wake Saleh Ally (kulia) na Makongoro Oging' (kushoto). • Yanga, Simba zamvutia lakini ashindwa kuchagua aipende ipi
• Asisitiza kama vipi, bora ziwe zinatoka sare kila mechi Chacha Makenge (36), ameishi katika handaki lililo katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa miaka minne. UNIA ina maajabu yake ndiyo maana wakasema, “tembea uone”. Katikati ya Jiji la Dar es Salaam, binadamu ameamua kuishi ndani ya handaki kwa miaka minne.

BREAKING NEWS: RAIS JAKAYA KIKWETE AMTEUA KAMANDA ERNEST MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA

Mkuu mpya wa jeshi la polisi Tanzania,Kamanda Ernest Mangu pichani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteua kamanda Ernest Mangu kuwa mkuu mpya wa jeshi la polisi Tanzania. Kamanda Mangu anachukua nafasi ya Inspekta jenerali Said Mwema ambaye anastaafu. 
Uteuzi wa kamanda Mangu unaanzia januari 1 2014.
CHANZO: ITV

RAIS KIKWETE, DK SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete (kulia) Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya leo. Jaji Warioba akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.AliMohamed Shein (kushoto) Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya leo.

PICHA YA LEO,JE UNAJIFUNZA NINI HAPA?

STYLES: UPANGILIAJI WA MAVAZI KWA WANAUME

STYLES: ONEKANA MTANASHATI KWA KUPANGILIA MAVAZI YAKO NAMNA HII

THE BEDROOM: MPANGILIO KATIKA CHUMBA CHA KULALA

Jukwaa la Katiba lampongeza JK

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba

Jukwaa la Katiba Tanzania limempongeza Rais Jakaya Kikwete na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuamua kufanya makabidhiano ya rasimu ya pili ya katiba hadharani.  Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu akiwa mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, alisema:

Wanaotumia vibaya laini za simu waanza kusakwa Dar

Twitter na Facebook


Hatimaye, Jeshi la Polisi nchini, limeanzisha operesheni maalumu ya kuwabaini na kisha kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook pamoja na laini za simu.
Jeshi la Polisi limeamaua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona teknolojia hizo zinatumiwa vibaya na watumiaji ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani ya nchi, kutishia usalama wa maisha ya watu na kutengeneza njama ovu za matukio ya kijambazi.

STYLES: LOAFERS ZA WANAWAKE

STYLES: ONEKANA NADHIFU KWA KUPANGILIA NGUO NAMNA HII

WASTARA NA WAIGIZAJI WENGINE WA FILAMU WAMSOMEA DUA MAREHEMU SAJUKI

Msanii wa filamu Wastara leo ameungana na wadau mbalimbali wa filamu makaburini Kisutu jijini Dar es Salaam kusoma dua kwaajli ya marehemu mume wake, Juma Kilowoko aliyekuwa maarufu kwa jina Sajuki.
Hata hivyo Wastara alisema baada ya shughuli ya leo(jana), dua rasmi ya marehemu Sajuki itafanyikia nyumbani kwao Songea, January 2, 2014.

HII NAYO KALI!

Polisi yanasa meno ya tembo ya 25m/= kwenye treni

Kaimu kamanda wa kikosi cha polisi cha Tazara, (SSP) Inocent Mgaya (katikati) akiwa na OCD wa kituo hicho SP, Bakari Makuka (kushoto) na SP, Shaaban Hussein wakionesha meno ya tembo 
Meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 25.5 yamekamatwa ndani ya treni ya Tazara katika stesheni ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro Vijijini,  yakisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Wazaramo: Kabila lenye sherehe lukuki, usipochangia, kushiriki unatengwa

watoto wakipongezwa na wazazi baada ya kutoka jandoni katika mkoa wa pwani. Picha ya Maktaba 
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na makabila zaidi ya 120, yaliyounganishwa na lugha moja ya taifa ambayo ni Kiswahili. Miongoni mwa makabila hayo ya Tanzania, limo Kabila la Wazaramo, ambalo linapatikana katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Wazaramo wametapakaa katika Wilaya za Kisarawe, Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga na Mafia.  Jijini Dar es Salaam, wengi wanaishi katika maeneo ya Buguruni, Magomeni, Ilala, Kariakoo na Msasani.

STYLES:MIKOBA MARIDHAWA YA WANAWAKE

STYLES: UPANGILIAJI WAMAVZAI YA JIONI