Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akihutubia vijana mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) aliyoizindua leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau toka timu ya Let us read Tanzania akimpa maelezo juu ya vitabu mbalimbali viliyotungwa na waandishi mashuhuri ndani na nje ya nchi.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza maswali mbalimbali watoto ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
====== ======== =======
RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ TANZANIA CAMPAIGN).
Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
11/10/2013.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa amezindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign) iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.