Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

Friday, 19 June 2015

DUNIANI KUNA MAMBO: VITUKO UGHAIBUNI: JAMAA AZIGAWA MALI ZAKE NUSU KWA NUSU BAADA YA KUMWAGANA NA MKEWE

Baiskeli iliyokatwa na jamaa huyo.
Gari hili nalo lilikatwa katikati kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya jamaa huyo na mkewe.
Video ya jamaa huyo akikata mali zake katikati

NJEMBA mmmoja nchini Ujerumani amezua sintofahamu baada ya kuamua kugawa nusu kwa nusu kila mali…
Baiskeli iliyokatwa na jamaa huyo

Gari hili nalo lilikatwa katikati kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya jamaa huyo na mkewe.
Video ya jamaa huyo akikata mali zake katikati.

Thursday, 28 November 2013

EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA





Na Sifael Paul
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.
Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.

Monday, 7 October 2013

MAHARUSI WATIWA MBARONI

Stori: Waandishi Wetu
JESHI la polisi nchini limefanikiwa kuisambaratisha ndoa ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mboga iliyopo Chalinze mkoani Pwani, Asha Daru mwenye umri wa miaka 15, aliyeozeshwa kwa Said Ally (29), mkazi wa Pugu jijini Dar, Ijumaa iliyopita.
Ndoa hiyo iliyotawaliwa na usiri mkubwa, ilifungwa nyumbani kwa bibi wa mwanafunzi huyo aitwaye Asha Abdallah maeneo ya Tandale Kwamtogole, Dar.
Kuvuja kwa siri ya ndoa hiyo kulifanikishwa na mmoja wa ndugu wa familia ya mwanafunzi huyo ambaye alidai kitendo hicho kilimkera hivyo kuwaomba mapaparazi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) iliyo chini ya Global Publishers kumnusuru binti huyo mdogo aliyedaiwa kulazimishwa kuolewa.
Baada ya kumsikiliza kwa umakini ndugu huyo mwenye mvi za hekima, mapaparazi wetu walilishirikisha jeshi la polisi na kuanza kuwafanyia mtego wa kuwanasa waliokuwa wakifanikisha tukio hilo.
BWANA HARUSI AWASILI UKWENI
Mishale ya saa 4:00 asubuhi kama ilivyoripotiwa na mtoa habari wetu, tayari bwana harusi ambaye ni fundi seremala alikuwa akiwasili ukweni na kupokelewa na nderemo za chinichini huku mapaparazi wetu wakiwa wamezingira eneo hilo.
Mapaparazi wetu walifanya upekepeke na kuingia hadi chumba cha bi harusi mtarajiwa na kumkuta shangazi yake akimpamba fastafasta kwa kile ilichoonekana kama walichelewa kumaliza kazi hiyo hadi ndoa inaanza kufungwa.
USTAADHI AMWAGA MAWAIDHA NA NDOA
Makachero wa jeshi la polisi na OFM, wakiwa kama wageni waalikwa, walisubiri kila kitu kiendelee ili kupata ushahidi wa tukio ambapo ustaadhi aliyekuwa akifungisha ndoa hiyo alionekana akimfungisha Said ambaye alitamka mbele ya waozaji na wageni wengine wakiwemo makachero kuwa anamuoa binti huyo kwa mahari ya shilingi laki tatu na nusu ambapo alilipa laki mbili na kubakiza deni la laki moja na nusu.
Baada ya tamko hilo, zilisikika nderemo za chinichini kutoka chumbani kwa bi harusi.
Huku nderemo zikiendelea, ustaadhi aliyekuwa akifungisha ndoa hiyo alianza kutoa mawaidha ya ndoa akiwausia maharusi kuishi kwa maadili ya kumpendeza Mungu na kuijaza dunia kama watajaliwa.

Saturday, 5 October 2013

MAMA LULU ATOBOA SIRI ZA KANUMBA

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Mama wa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila kwa mara ya kwanza amemfungukia marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Marehemu Steven Kanumba.
Katika mahojiano rasmi na Risasi Jumamosi, juzi jijini Dar, Mama Lulu aliweka wazi kila kitu kuhusu madai mbalimbali ya yeye na mama Kanumba, Lulu na marehemu Kanumba.
Mambo yaliyoelekezwa ayajibu mwanamama huyo ni pamoja na madai kwamba alishapokea barua ya posa ya Kanumba kutaka kumuoa Lulu, yeye na mama Kanumba kugombana hivi karibuni na Lulu kumjali zaidi mama Kanumba kuliko yeye.
Awali, mwanamke huyo alisema miongoni mwa watu waliofiwa na Kanumba yeye yupo mstari wa mbele kwani uchungu alioupata siku ya tukio mpaka leo haujamtoka.
Mahojiano kamili yalikuwa kama ifuatavyo:
Risasi: Mama kuna madai kadhaa ambayo ni vyema uyajibu.
Mama Lulu: (Kwa ukali kidogo) maswali gani? Mimi sitaki waandishi, nilishasema! Kama ni kuhusu Lulu muulizeni mwenyewe.
Ilibidi waandishi watumie kazi ya ziada ili mama huyo aweze kuzungumza.
Risasi: Ni mambo ya kawaida tu mama, wewe ndiyo unafaa kujibu, tafadhali tusikilize.
Mama Lulu: Haya, ulizeni.
Lucresia Karugila.
ALIUJUA UHUSIANO WA KANUMBA NA LULU?
Risasi: Kuna madai kwamba uliujua uhusiano wa kimapenzi kati ya Lulu na Kanumba,  lakini mama Kanumba alikuwa hajui kinachoendelea, ni kweli?
Mama Lulu: Kwanza katika maisha yangu hakuna siku niliyowahi kupata mshtuko kama niliposikia Kanumba amefariki dunia na mwanangu Lulu kahusishwa na kifo kile, nilishtuka sana.
“Ilikuwa mara yangu ya kwanza kujua kumbe Kanumba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanangu Lulu, lakini kabla ya hapo sikuwa najua lolote.

Saturday, 21 September 2013

PEPO LA UBAKAJI...TUTALIMALIZAJE?

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
PEPO la ubakaji linazidi kutikisa jamii ambapo hivi karibuni watoto wawili wanaripotiwa kubakwa kwa nyakati tofauti jijini Dar.
Mtoto mmoja, mkazi wa Kitunda (jina linahifadhiwa) amebakwa na mfanyakazi wa kufuga nguruwe aishie maeneo ya jirani baada ya kumrubuni binti huyo mwenye umri wa miaka 6 kuwa atamnunulia pipi.

Akizungumza kwa uchungu, baba wa mtoto huyo, Joseph Isaac alisema mwanaye alibakwa na mfanyakazi huyo wa nguruwe aliyemtaja kwa jina la Fabiano baada ya kumuahidi kuwa atampa pipi.
“Siku hiyo nilirudi nyumbani nikamkuta mwanangu anachemka homa kali, nikamwambia mama yake amuogeshe tumpeleke hospitali kwani tulikuwa tumeshampatia dawa ya kutuliza lakini haikumsaidia,” alisema baba huyo.

MAJANGA MENGINE HAYA: BINTI MIAKA 16 AOLEWA, ASIMULIA RAHA YA NDOA

Stori: Denis Mtima na Chande Abdallah

BINTI wa miaka 16, Husna amefungukia ndoa yake na mwanaume anayetajwa kwa jina la Juma na kudai anafurahia ndoa yake, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.
Akizungumza na waandishi wetu, Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Husna alisema aliolewa na mwanaume huyo Julai mwaka huu, mkoani Lindi na mwezi uliopita walihamia Dar.

Mume wa Husna anayetafutwa, Bw. Juma
Alipohojiwa kwa nini alikubali kuolewa akiwa na umri mdogo, alisema kwamba alikosa kazi ya kufanya.
Binti huyo aliwashangaza waandishi na polisi pale alipodai kwamba yeye si mtoto mdogo kwani ana mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 ambaye ameolewa na amezaa mtoto hivyo yeye asikodolewe macho.
“Mbona mdogo wangu ana miaka 15 ameolewa. Mimi siyo mtoto mdogo ninaijua raha ya ndoa yangu,” alisema Husna.
Waandishi wetu walipotaka kujua kama huwa anapatwa na maumivu anapokutana na mumewe,  alisema anajisikia kawaida kwani alianza mapenzi tangu akiwa shuleni. 
Kama vile haitoshi, binti huyo alisema kuwa huwa anawashangaa hata polisi ambao wanajaribu kulifuatilia suala hilo.
Hata hivyo, Husna alisema kuwa angependa kuendelezwa kimasomo kama akipatikana mfadhili na kuachana na mumewe huyo.
“Nipo tayari kuachana na mume wangu na kwenda kusoma kwa kuwa umasikini ndiyo uliochangia kuolewa mapema,” alisema.
Awali waandishi wetu walipewa taarifa za kuwepo mwanaume aliyeoa mtoto mdogo na majirani wa wanandoa hao na kuwataka kulivalia njuga suala hilo.
”Tunashangaa mwanaume amemuoa binti mdogo sana yaani sawa na mwanaye kabisa. Muda mwingi binti anachezea michanga na watoto wengine. Sijui kamtoa wapi?” alisema mmoja wa majirani hao.

Thursday, 19 September 2013

MATESO 100%


Kwa aayetaka kumsaidia aaweza kufanya hivyo kupitia namb0654 880707.

Stori: Gladness Mallya na   Hamida Hassan
HAYA ni mateso 100%! Dereva mmoja wa boda boda mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salamaa anayejulikana kwa jina la Joseph Nyunza, yupo katika mateso makali yaliyosababishwa na Sangoma aliyeng’oa vyuma alivyowekewa hospitalini na kusababisha mguu wake kuoza.
Akizungumza na gazeti hili akiwa hoi kitandani nyumbani kwa shangazi yake, Joseph alisema awali alikuwa dereva wa pikipiki lakini Julai mwaka huu, alipata ajali maeneo ya Kimara Suka jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na gari lililohama njia na kumvunja mguu wake wa kulia.
Baada ya kupata ajali hiyo, alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipokelewa na kupelekwa katika kitengo cha mifupa (Moi) ambako baada ya kufanyiwa vipimo, iligundulika kuwa mfupa mkubwa wa mguu wake ulivunjika, hivyo kuwekewa vyuma ‘antena’ ili uweze kuunga. Aliruhusiwa kurudi nyumbani huku akitakiwa kurejea tena hospitalini kwa ajili ya upasuaji.

JOHARI, CHUCHU HANS WAZICHAPA



Stori: Brighton Masalu

KIMENUKA! Waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wanadaiwa kuchapana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Amani limenyetishiwa mkanda kamili.


Blandina Chagula ‘Johari’
TUHUMA

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu wa wasanii hao, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ofisi za RJ Productions, zinazomilikiwa kwa ubia wa Ray na Johari zilizopo Sinza-Mori jijini Dar ambapo Johari alikuwa akimtuhumu Chuchu mambo mazito ya kimapenzi kwa Ray.
Shushushu huyo alitonya kuwa, siku ya tukio Johari na wasanii wenzake walikuwa wakirekodi filamu ndani ya hoteli moja (jina tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo ndipo alipofikishiwa umbeya kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi hizo ‘akijiachia’ na bosi mwenzake (Ray), jambo lililotia ganzi moyoni mwa mdada huyo.


Chuchu Hans.
MCHEZO MZIMA

‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kuwa baada ya Johari kupata habari hizo, bila kujiuliza wala kuvuta subira, ‘alisaga soli’ hadi maeneo hayo.
“Alipofika aliingia ndani moja kwa moja na kumvamia Chuchu huku akimshushia kipigo chenye ujazo,” kilidai chanzo hicho.
Alidai kuwa katika timbwili hilo, Chuchu naye alifurukuta ndipo wakazichapa laivu kabla ya Ray aliyekuwa nje kusikia na kuwahi kuokoa jahazi.
“Unajua kilichomshtua Ray ni kilio cha Chuchu aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuzidiwa na Johari,” kilidai.

MZEE MAJUTO AITWA BAKWATA


Stori: Imelda Mtema
SIKU chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman ‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake, Amani liko mbele kukuhabarisha.
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto, Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.
Akasema akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji:  “Kwani huyo Rehema ndiye aliyenioa?”
Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.
Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.

Tuesday, 17 September 2013

KIJIJI CHA UNGA CHAFUMULIWA

Stori: Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
JIJI la Dar es Salaam lina mambo mengi lakini moja ambalo linatisha ni kugundulika kwa kijiji cha madawa ya kulevya ambacho kipo kando ya Bahari ya Hindi.
Mwili ulioshonewa madawa ya kulevya.
Kijiji hicho ni Kunduchi, nje kidogo ya jiji na uchunguzi wa gazeti hili umeonesha kuwa, madawa ya kulevya yenye thamani ya mabilioni ya shilingi yamekuwa yakikamatwa katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Uwazi kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema matajiri wengi wa ‘unga’ wamekuwa wakitumia eneo hilo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni salama kwa shughuli hiyo.
Kijiji cha dawa za kulevya kilichopo Kunduchi jijini Dar
“Hapa Kunduchi ni kando ya bahari, wengi wanatumia majahazi au boti za uvuvi kuingiza mihadarati hiyo. Wanapoleta madawa yao wanaonekana kama wanatoa samaki au mizigo mingine ya kawaida lakini kumbe ni madawa ya kulevya,” alisema kijana mmoja.
Mzee wa siku nyingi wa kijiji hicho alisema anasikitishwa kuona kuwa kitongoji chao kimekuwa makao makuu ya biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya na yanauzwa wakati serikali ipo.
“Kuna wakati tulitaka sana kijengwe kituo cha polisi lakini tukaambiwa kuna matajiri hawataki hilo, hivyo ajenda hiyo ikaisha na wengi tunaamini matajiri kwa kutumia fedha hawaruhusu kituo cha polisi kuwepo eneo hilo ndiyo maana hakijengwi,” alisema mzee huyo na kuongeza kuwa Kituo cha Polisi cha Silver Sands kiko mbali sana.

KIGOGO MAGARI YA WIZI ANASWA

Stori: Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
Jengo ambalo linadaiwa ndiyo kiwanda hatari cha kubadilisha magari ya wizi, kimefumuliwa na mmiliki wake sasa hivi yupo nyuma ya nondo akingoja kufikishwa mahakamani.
Kigogo wa magari ya wizi, Benovilla Luhanga baada ya kunaswa.
Benovilla Luhanga, 43, ametajwa kuwa ndiye mmiliki wa kiwanda hicho na siku ananaswa, alikutwa na magari ya kihafari matano ambayo yote inadaiwa ni ya wizi.
Vilevile, Luhanga alikutwa na Bajaj moja ambayo imedaiwa nayo ni ya wizi na kwamba alikuwa tayari ameshaibadili rangi.
Luhanga alikamatwa akiwa na mkewe ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Moja ya gari alilokutwa nalo mtuhumiwa.
Kigogo huyo na mkewe, wanaishi ndani ya nyumba hiyo iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, kwa nje huonekana kama gereji lakini ndani ni makazi ya watu na shughuli za ubadilishaji magari, Bajaj na pikipiki hufanyika humo.
Luhanga na mkewe walikamatwa baada ya polisi kuvamia kiwanda hicho, saa 5 asubuhi lakini mchakato wa ukamataji ulikamilika saa 10 alasiri.
Mchakato wa kuwakamata uliwagharimu polisi jumla ya saa 5 kukamilika kwa sababu ilibidi kufanya upekuzi wa hali ya juu kwenye kiwanda hicho ili kubeba kila kitu kilichoonekana ni cha wizi.
Magari yote yaliyokutwa kwenye kiwanda hicho pamoja na Bajaj moja, ilidaiwa ni mali za wizi huku tayari yakiwa yameshabadilishwa rangi na kufungwa namba feki za usajili, isipokuwa gari moja.

Saturday, 14 September 2013

IRENE UWOYA AMSHUKIA SHIGONGO





UDAKU WA LEO: UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU!

Na Waandishi Wetu
MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
MAMBO yanaendelea kumwendea kombo mwigizaji huyo huku akiwa ameanza kuporomoka vibaya kwenye sanaa na kujikuta akiingia  matatani kwa tuhuma za aibu.
HABARI ZA KIPOLISI
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.
MMILIKI AMWANIKA UWOYA
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.
“Nilirejea hapa nchini nikiwa na simu hiyo. Tena unajua simu yenyewe ni ya kisasa, toleo la mwaka huu,” alisema Mohammed.Alisema Agosti 23, mwaka huu, akiwa kwenye gari katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Nyamwezi, Kariakoo, Dar aliibiwa simu hiyo na mtu asiyemtambua.

Friday, 13 September 2013

DUNIANI KUNA MAMBO! HII NI BABA LAO!

Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
MDOSI au Kanjibai aliyefahamika kwa jina moja la Milah ambaye ni bosi wa kampuni moja ya ujenzi yenye makao yake Mwenge jijini Dar alinaswa chooni akiwa na mfanyakazi wake, John Carlos ‘Shabani’ (watu walimpachika jina la Shabani kutokana na Kanjibai wa kwenye Komedi) ikidaiwa walikuwa katika mazingira ya ulawiti, Ijumaa ‘Kubwa’ lina sinema yote.
...Choo walipokuwa wamejifungia Milah 'Kanjibai' na John Carlos ‘Shabani’.
Ishu hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wawili hao walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia usumbufu watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.
KISA KILIPOANZA
Siku hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers, Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo. Alisema:
“Jamani hebu njooni haraka hapa kwenye hii kampuni ya ujenzi ya… (jina lipo) iko hapa Mwenge. Kuna bosi wetu mmoja amejifungia chooni na mfanyakazi mwenzetu kwa zaidi ya robo saa sasa, sijajua nini kinaendelea humo ndani. Sisi wengine hapa matumbo ya kuendesha yametushika sijui tufanyaje?!”

KANIKI ATINGA MAHAKAMANI

Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Joseph Kaniki amepandishwa kizimbani jijini Addis Ababa, Ethiopia kutokana na tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya.
Iwapo Kaniki pamoja na mwenzake Mkwanda Matumla ambaye ni bondia watapatikana na hatia, basi watafungwa nchini Ethiopia hadi watakapomaliza kifungo chao, Serikali ya Tanzania imethibitisha hilo.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo ameliambia Championi Ijumaa, jana kutoka Addis Ababa kuwa, Kaniki na Mkwanda walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza  mwanzoni mwa wiki na huenda ikawa hivyo tena wiki ijayo.
“Jana (juzi) tulikwenda kuwaona na tumekuwa tukifuatilia kwa karibu, huku kidogo kuna utaratibu tofauti, hivyo hatujajua lini watapandishwa tena kizimbani kwa mara ya pili.
“Iwapo watapatikana na hatia, kama ni kifungo cha jela, basi watatumikia hapa Ethiopia. Maana tunabanwa kutokana na kutokuwa na mkataba wa kupeana washitakiwa au wafungwa kama ambavyo nilieleza awali,” alisema Shelukindo.

Thursday, 12 September 2013

NDOA YA MZEE MAJUTO YAVUNJIKA

Na Imelda Mtema
MWANAMKE anayedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchekeshaji mahiri Bongo, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto au King Majuto, Rahma Abdallah (20), ameibuka na kudai kutelekezwa na mumewe huyo.
Mzee Majuto akiwa na mkewe Rahma Abdallah siku ya ndoa yao.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri jijini Dar Julai 28, mwaka huu na kudumu siku 44, inaonekana imevunjika rasmi baada ya Mzee Majuto kutoa talaka kupitia kwa msanii wa filamu aitwaye Rehema Omary.
WOTE NI WAJA LEO, WANDOKA LEO
Akizungumza na gazeti hili katika ofisi zetu, Bamaga-Mwenge, Dar, Septemba 9, mwaka huu, Rahma alidai kuwa alikutana na Mzee Majuto jijini Tanga na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita kabla ya kufunga ndoa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliopita.
“Tulifahamiana Tanga, mimi ni mwenyeji wa huko kama ilivyo kwa Mzee Majuto, wakati tukiwa kwenye uhusiano, ulipofika Mwezi wa Ramadhani akaona bora tufunge ndoa ili tusiendelee kutenda dhambi, akaniambia dhamira yake hiyo nami sikukataa,” alisema Rahma.
Rahma Abdallah (20).

LULU APATA VITISHO

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Stori:  Jelard Lucas
KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.

Wednesday, 11 September 2013

WATU WENGINE BWANA,HAWANA HATA AIBU!DENTI ALIYEDAI KUZAA NA DIAMOND... AUMBUKA, ATISHIA KUJIUA

Video: Sasha siku alipokuwa akiongea na GPL kuhusu madai ya kuzaa na Diamond.
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha Juma akiongea na GPL..
Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond, ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana.
Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua.

Tuesday, 10 September 2013

SAKATA LA MBWANA MATUMLA KUNASWA NA UNGA.

Stori: Makongoro Oging’ na HarunI Sanchawa
TAARIFA za kushangaza kwamba bondia maarufu nchini, Mbwana Matumla amekamatwa na madawa ya kulevya nchini Uswisi mara Hispania sasa ni kama sinema.
Madawa ya kulevya.
Awali ilidaiwa kuwa, Mbwana alidakwa nchini Hispania akiwa njiani kuelekea Italia kupeleka mzigo huo ambao mpaka sasa taarifa hizo bado ni kizungumkuti.
Baadaye kwa kupitia vyanzo vyetu toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania ikadaiwa kuwa, bondia huyo alikamatwa kwenye mpaka wa nchi ya Ujerumani na Switzerland (Uswisi) akiwa na kilo tatu za ‘unga’ aina ya heroin wenye thamani ya shilingi 150,000,000 za Kitanzania.

Monday, 9 September 2013

KIMENUKA: STRAIKA SIMBA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Madawa ya kulevya.
Na Mwandishi Wetu
SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba (jina tunalihifadhi kwa sasa), kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, amekamatwa na madawa ya kulevya siku tatu zilizopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia.

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...