Wengi hatujui haki zote na hii hupelekewa mtu kuonewa bila sababu. Soma hapa ujue haki zako uwapo mikononi kwa polisi.
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi
muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa
mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini
anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa
kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya
kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji
anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati,
kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.