Showing posts with label VIDEO. Show all posts
Showing posts with label VIDEO. Show all posts

Sunday, 10 January 2016

DINA MARIOS:KATIKA MAISHA HAKUNA HALI YA KUDUMU

Nimependa sana hizi video za Dina Marios kwani zinaeleza ukweli halisi wa maisha tunayoishi na tunavyogeukwa na watu tuliowapenda na kuwajali. Hii huwa ni somo na njia ya kukuondoa katika level moja kwenda nyingine.Inaweza ikawa una mawazo mengi ambayo ukiyafanyia kazi unabadilisha kabisa maisha yako.Tuchukulie yale yote yanayotutokea kama njia ya kubadilisha level za maisha tuliyokuwa tunaishi awali kutoka misha yasiyoeleweka na kuishi maisha ya kueleweka na yaliyo bora zaidi.Ni video za kuangalia na utajifunza kitu. Asante sana Dina kwa ukweli uliouandika.

Tuesday, 14 April 2015

WANAWAKELIVE: VILIO VYA WANAWAKE WAJANE KUDHULUMIWA MALI WALIZOCHUMA NA WAUME ZAO



Nadhani ni wakati mwafaka wa kuwa na taasisi/vyombo vingi visivyo vya kiserikali ili kushughulikia maswala ya sheria za mirathi kwa wanawake wajane. Inasikitisha kuona mwanamke amechuma mali na mumewe kwa taabu ndugu za mume wakiwa na yao halafu anapofariki mume wao wanajileta kurithi mali.Mali ipi hapa? Jamani watu hawana aibu hivi. Marehemu kaacha mke na watoto wake na hao ndiyo warithi halali wa mali. Sasa hawa ndugu za mume wakichukua mali ambayo wala hawakuichuma,watoto wataishi vipi? Watu waache kubweteka na kusubiri mali za kurithi.
Nimeupenda ujasiri wa mwanamke wa mwisho katika video hiyo hapo juu.Yeye aliamua kukomaa na wapenda vya bure.Tuwasaidie wale wasioelewa haki zao.
Mwanaume jasiri hutafuta mali yake mwenyewe kwa jasho lake na mtegemea cha ndugu siku zote,hufa masikini.

Badilikeni!

Tuesday, 7 April 2015

Survivor Tales; Cynthia Cherotich who lived to tell her tale


 Cynthia Cherotich was certainly one of the lucky ones, who managed to walk off the Garissa University College campus after Al shabaab militants massacred over 140 of her colleagues.Victoria Rubadiri with her story of unbelievable resilience and hope to live another day.

Wednesday, 11 February 2015

YEMI ALADE - JOHNNY



Johnny leaves me follow Cynthia
And i don’t know what to do
And he talk say i no do am
Like the way Cynthia dey do

Saturday, 22 November 2014

JE, HALI YA ELIMU MJINI TANGA IKOJE?



Nimefurahi kuwaona walimu wangu wakiongea katika video hii.
Wa kwanza ni Mrs Rajyagur, ambaye alikuwa mwalimu wangu wa kiingereza katika shule ya msingi  Darajani(zamani Agakhan),Tanga.

Na wa pili ni mwalimu Mwaeshu,ambaye alikuwa ni mwalimu wangu wa Kiswahili katika shule ya sekondari,Usagara.

Wednesday, 4 June 2014

MJUE MECK KHALFAN,MTANZANIA ALIYEGUNDUA CHARGER KWA JINA LA "PUKU"

Kama unatarajia kuwa katika mazingira ambayo hakuna umeme wa uhakika hasa 
kwa wale wenye iphone, tablets na kifaa chochote kinachochajiwa kwa kutumia usb |"PUKU" ndiyo mpango mzima.Sikiliza vizuri hapa kwa kuelewa vizuri.



PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...