Stori hii nimeikuta jamii forums nikaona ni vizuri kuiweka hapa
Kadri siku zinavyokwenda na ugumu wa maisha unavyozidi, ndivyo hivyo hivyo kunavyoibuka kada mbalimbali za matapeli na mbinu mpya za utapeli wa kujipatia kipato!.
Mimi ni mkazi a Mbezi Juu, jirani na Hospitali ya Masana, leo nimetoka Church niko home naangalia marudio ya tamthilia ya Isidingo, nasikia mlio wa boda boda imesimama nje, kisha mtu akabisha hodi, namtuma mtoto akafungue, akarudi kuniambia kuna mgeni ananiita nitoke nje, nikamtuma amkaribishe aingie ndani, jibu likaja mwambie tuu baba atoke, kuna jambo la dharura!.
Showing posts with label TAARIFA. Show all posts
Showing posts with label TAARIFA. Show all posts
Thursday, 10 September 2015
Friday, 17 July 2015
SHINDANO LA BLOG
Kwa wote mnaoshiriki shindano la blog hongereni sana.Utaratibu ni kuwa hatujibu chochote kama umepatia kujibu swali. Kila la heri kwenu wote.
Anna
Mmiliki wa blog
Friday, 17 April 2015
HABARI ZA PUNDE: AJALI NYINGINE YAUWA 19 MBEYA LEO
Ajali za Tanzania kwenye vichwa vya habari zimezidi kuongezeka, leo April 17 2015 ajali nyingine imetokea Mbeya baada ya gari la abiria kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni Mbeya.
Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa Polisi Mbeya zinasema waliofariki mpaka sasa ni 19, endelea kukaa karibu na millardayo.com kwa taarifa zaidi.
PICHA ZAIDI
Wednesday, 26 November 2014
MAJAMBAZI WAVAMIA SUPER MARKET, STOCKHOLM,SWEDEN
Majira ya saa 11 jioni jana,watu wawili wenye silaha, walijaribu kupora katika supermarket iitwayo Coop Konsum eneo ninaloishi. Waporaji hawakufanikiwa kupora bali walimjeruhi kwa risasi muuzaji wa kike wa supermarket hiyo.
Source: Aftonbladet
Monday, 10 November 2014
TUSAIDIANE KATIKA KUBORESHA BLOG YETU
Blog hii ipo kuelimisha zaidi na ndiyo maana tunatumia muda mwingi kuwaletea vitu vya kuwapa mwanga katika nyanja tofauti kupitia trend zetu tofauti mfano:
- the wardrobe-huonyesha uvaaji,
- the living room-huonyesha urembaji wa sebule kuanzia samani,rangi,mapambo n.k
- the dining room-urembaji wa dining kuanzia samani, mapambo,rangi na vyombo,
- the kitchen-tunaonyesha jinsi ya kudesign jiko, vifaa vya jikoni, upambaji wa jiko n.k,
- the garden/container gardening-jinsi unavyoweza kubuni bustani nje na ndani ya nyumba yako, urembo wa kucha-jinsi unavyoweza kutengeneza kucha zako mwenyewe, urembeshaji wa kucha n.k
- urembo wa hina-michoro tofauti ya hina miguuni, mikononi n.k
Tunawaomba wasomaji wetu na wale wote ambao mnavutiwa na kazi yetu mtupe support ya hali na mali ili tuendelee kuwaletea mambo mazuri.Kuna mambo mengi mazuri yanakuja hivyo mtajua kupitia humu.
Tunakaribisha matangazo kwani nafasi tunayo kubwa.Vile vile kwa anayetaka kuchangia uendeshwaji wa blog iwe kampuni au mtu binafsi,unaweza kufanya hivyo kupitia kitufe "donate",kilichopo juu kabisa,upande wa kulia mwa blog, ili kuchangia kiasi chochote.
Tunatanguliza shukrani.
Anna Nindi
k.n.y Rainbow-tz blog
Thursday, 16 October 2014
HEKA HEKA ZA VITAMBULISHO VYA URAIA JIJINI TANGA
Wakazi wa maeneo ya Usagara Tanga na viunga vya jirani,wakiwa wamepanga foleni kujiandikisha kupata vitambulisho vya uraia.Kama na wewe ni wa maeneo hayo wahi katika kituo kilichopo nyumba za bandari au shule ya sekondari, Usagara.
Saturday, 19 July 2014
KUHUSU MTOTO ALIYEPOTEA KWENYE MAZINGIRA YA KUTATANISHA DAR ES SALAAM
Sasa Gea Habib na idara ya Hekaheka wameenda mpaka huko kwao na huyo mtoto,sikiliza kilichozungumzwa.
88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora.
Bonyeza play kusikiliza.
Chanzo: Millard Ayo
Sunday, 8 June 2014
BREAKING NEWS: MSANII MZEE SMALL,AFARIKI DUNIA
Muigizaji
mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki
dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda
mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu
aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small.
MUNGU AILAZE ROHO YA
MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
CHANZO: GPL
Sunday, 1 June 2014
HABARI ZA KUSIKITISHA: MTOTO ALIYEWEKWA KWENYE BOKSI MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA

Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi.
Saturday, 31 May 2014
MWONGOZAJI WA VIPINDI NA FILAMU GEORGE TYSON, AFARIKI DUNIA
George Tyson enzi za Uhai wake
Taarifa zilizotufikia katika meza yetu ya habari Usiku huu ni kuwa Muongozaji mahiri katika Tasnia ya Filamu nchini na Mzazi Mwenza wa Msanii nguli wa Filamu nchini Vyonne Cherry Au Monalisa, Bwana George Tyson amefariki dunia mara baada ya kupata ajali ya gari Mkoani Morogoro Katika eneo la Gairo wakati wakitokea Mkoani Dodoma ambapo walienda kwaajili ya Kuadhimisha Miaka Miwili ya Kipindi Cha Mboni Show.
Wednesday, 28 May 2014
MSHAIRI MASHUHURI NA MWANDISHI WA VITABU, MAYA ANGELOU KUTOKA MAREKANI,AFARIKI
PICHA: Rais Barack Obama akimkumbatia Maya Angelou baada ya Maya kupata "medal of Freedom”, 2010.
Mshairi, Mwandishi na mwanaharakati mashuhuri,Maya Angelou amefariki akiwa na umri wa miaka 86. Habari hizi ni kwa mujibu wa kituo cha WGHP-TV kutoka katika mji wa Winston-Salem ambapo Maya anatokea.
Tuesday, 27 May 2014
MSANII WA BONGO MOVIE RACHEL HAULE AFARIKI
Msanii Rachel Haule
Msanii wa
Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari
zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere,
zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya
kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU
ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
|
Monday, 19 May 2014
DIAMOND MPAKA SASA AONGOZA KURA ZA BET KWA KUNDI LA WASANII WA AFRIKA
Msanii Nasibu Abdul alias 'Diamond Platnumz' kwa sasa anakimbiza katika mchakato wa upigaji kura katika Tuzo za BET 2014 akifuatiwa na Mafikizolo. Tuzo hizo zitatolewa Juni 29 mwaka huu jijini Los Angeles, Marekani.
Na jina la Diamond lipo katika kipengele "BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA" bofya tundu lenye jina lake kisha bofya "VOTE".
Kama ulikuwa hujapiga kura fanya hivyo sasa ili tuzo hii ije Tanzania!

Kama ulikuwa hujapiga kura fanya hivyo sasa ili tuzo hii ije Tanzania!
Thursday, 8 May 2014
BRINGBACK OUR GIRLS

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA MPYA WA TRA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Kulingana
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza
tarehe 06 Mei, 2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla
ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-
Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.
Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.
Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).
Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014
Tuesday, 22 April 2014
HAPPY BIRTHDAY RAINBOW-TZ KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA!

Tarehe
21-04-2014 blog hii ilitimiza mwaka mmoja toka iingie hewani.Kwa niaba ya rainbow-tz
blog,ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote wanaofuatilia
matukio mbalimbali yanayowajia kupitia rainbow-tz blog kwani utembeleaji
wenu katika blogu hii ndiyo unatupa moyo kuendelea kuwaletea posti mbalimbali
zenye kuelimisha.
Thursday, 17 April 2014
MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.
Sunday, 13 April 2014
MUHIDINI GURUMO AFARIKI
Maalim Muhidin Gurumo enzi za uhai wake.
MKONGWE wa Dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo aliyekuwa akitumikia Bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ kabla ya kustaafu mwaka jana, amefariki dunia.
Kwa mujibu wa habari tulizozipata kupitia chanzo chetu, Mwanamuziki huyo amefariki alasiri hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mpaka sasa sababu ya kifo cha Mzee Gurumo bado haijajulikana na taratibu za mazishi bado hajizafahamika.
(HABARI NA DEOGRATIUS MONGELA / GPL)
|
Wednesday, 9 April 2014
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
Mamlaka ya Mawasiliano imebaini kuwa kuna mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti inayojiita “TCRA Foundation” na inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PALM TREES ARE BEAUTIFUL
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...

-
Dar es Salaam: Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JN...
-
1. PASTA Hiki ni chakula cha haraka.Unaweza kutayarisha pasta kwa kuongeza tu protini ulizonazo katika jokofu lako mfano kuku...
-
No 10 : Oriens By Van Cleef & Arpels No 9 : Love Sweet Love By Philosophy Love Sweet Love by Philosophy is an ideal summer perfum...